Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake umeanza kuisadia Serikali ya Indonesia kufanya tathmini namna matukio ya tsunami na mlipuko wa volcano ilivyowaathiri wananchi wa eneo hilo.
Katibu mkuu wa mkataba wa biashara ya kimataifa kwa viumbe vilivyo hatarini Flora na Fauna CITES leo ametangaza kuwa amefanya uamuzi wa kuitunuku serikali ya Thailand kwa juhudi za kulinda viumbe hao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema taarifa za karibuni za kutimuliwa wakimbizi zaidi ya 150 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Angola huenda likazua wimbi jipya la kurejeshwa kwa nguvu wakimbizi katika nchi hizo mbili.
Mwanasoka mashuhuri duniani Didier Drogba leo ameanza kampeni ya kimataifa ya kutanabaisha jinsi uchaguzi huru na wa haki unavyoweza kuwa nyenzo muhimu ya kuzitoa nchi masikini kabisa duniani kutoka kwenye ufukara huo.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulia masuala ya haki za binadamu amesema kuwa nyaraka iliyofichua vita vya Iraq, imefumbua namna haki za binadamu zilivyokiukwa na kuleta udhalilishaji mkubwa kwa utu wa binadamu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO leo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya urithi wa sauri na picha limetoa wito wa kuongeza juhudi za kuhifadhi kumbukumbu muhimu zilizoko katika njia ya sauti na picha.