Wanawake

Ubunifu wa wanawake wabadili jamii zao #WorldIPDay

Ubunifu wa wanawake katika nyanja mbalimbali kuanzia mavazi, tiba na hata ufugaji sasa unadhihirisha kuwa udadisi wa kundi hilo ukijengewa uwezo, umaskini utasalia historia.

Uchuuzaji mboga wanusuru wanawake dhidi ya umaskini Uganda

 Umoja wa Mataifa  unahimiza kuleta   maendeleo kupitia malengo yake ya maendeleo endelevu SDGs.Mathalani   lengo namba moja la kutokomeza  umaskini kwa ifikapo mwaka wa 2030. Kwa mantiki hiyo wanawake wa wilaya ya Lwengo, Kusini mwa Uganda nao wameamua kujifunga kibwebwe kuweza kutokomeza umaskini .  Wameanzisha soko lao ambalo linauza bidhaa mbalimbali za matunda kama vile nyanya , na mboga za majani. Siraj Kalyango amevinjari eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya wanawake hao na kutuandalia Makala ifuatayo.

Mimba za utotoni ni zahma kwa wasichana na jamii

Mimba za utotoni ni changamoto kubwa nchini Tanzania na hususani katika maeneo ya vijijini.  Serikali ya nchi hiyo ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, ustawi wa jamii na mashirika ya kitaifa na kimataifa kama la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wanaelimisha jamii wakiwemo wasichana wadogo mashuleni athari za mimba hizo. 

Okoa mwanao kwa kumnyonyesha miaka 2 mfululizo- WHO

Mtoto anaponyonyeshwa miaka miwili mfululizo bila kupatiwa kimiminika chochote ataepusha gharama kubwa zinazotumika kutibu magonjwa kama vile kuhara, magonjwa ambayo husabaisha na matumizi ya maji yasiyo safi na salama katika kumwandalia maziwa mbadadala badala ya yale ya mama.

 

Polisi wanapomwepusha msichana na FGM

Ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake unasalia kuwa ni jambo linalotishia tu siyo afya ya kundi hili bali pia maendeleo yao ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Sasa watoto wenyewe wa kike wanasimama kidete kuhakikisha hawakumbwi na kikwazo hicho.

Kumuwezesha mwanawake ni kuwezesha maendeleo : Sofia Donald

“Wanawake wakijengewa uwezo kiuchumi wataweza kukabiliana na matatizo mbalimbali katika jamii inayowazunguuka ikiwemo suala la tabianchi na mazingira  na pia ukatili wa kijinsia”

Wanawake na wasichana wenye Usonji wasiachwe na treni ya 2030

Usonji hukwamisha maendeleo ya mtoto na anapokuwa wa kike basi hali inakuwa mbaya zaidi.