Wanawake

Ofisa wa UNRWA anasema hali Ghaza ni ya kutisha mno

John Ging, Mkurugenzi wa Operesheni za Shirika la UM la Kufarajia Wahamiaji wa KiFalastina kwenye Mashariki ya Karibu (UNRWA) ameiambia Ofisi ya UM, Geneva, hii leo, kwa kutumia njia yasimu, ya kwamba mipangilio ya kuhudumia misaada ya kihali Ghaza, kwa umma muhitaji, imevurugwa kwa sasa, kwa sababu ya kuendelea kwa mapigano, hali ambayo vile vile alisema imeongeza khofu na wasiwasi miongoni mwa wakazi wa Ghaza pamoja na umma wa eneo jirani.

Watoto wa Ghaza lazima walindwe, Kamati ya Haki ya Mtoto yasihi

Kamati ya UM juu ya Haki ya Mtoto, yenye wajumbe 18, ambayo inakutana sasa Geneva, imetoa ripoti yenye kubainisha wasiwasi mkubwa juu athari haribifu, kiakili, dhidi ya watoto wadogo, kutokana na vurugu la mapigano liliopamba kwenye eneo la Tarafa ya Ghaza.

LRA inaendelea kutesa wasio hatia katika JKK

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza kukhofia usalama, na hali, kijumla, kutokana na mashambulio ya karibuni ya kundi la waasi wa Uganda la LRA kwenye Jimbo la Orientale, katika JKK.

Haki za binadamu zakiukwa Ghaza, inasema UM

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu baada ya majadiliano ya siku mbili, kwenye kikao cha dharura, Ijumatatu mjini Geneva limepitisha azimio lenye kulaani vikali operesheni za kijeshi zinazoendelea sasa hivi za vikosi vya Israel kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Ghaza.

WFP kuanzisha operesheni za kuokoa maisha ya mamia elfu Ghaza

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanzisha huduma ijulikanayo kama Operesheni za Kamba ya Kuokolea Ghaza, yenye lengo la kuhudumia watu wenye njaa ambao idadi yao inaendelea kuongezeka kila kukicha, tangu Israel kuanzisha mashambulio yake karibu wiki tatu zilizopita.

Kamati ya Haki ya Mtoto yakutana Geneva

Kamati juu ya Haki ya Mtoto imeanzisha kikao cha 50 mjini Geneva leo Ijumatatu kuzingatia ripoti kuhusu utekelezaji wa haki hizo katika mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea ya Kaskazini), JKK, Malawi, Uholanzi, Chad na vile vile Moldova

UNRWA inasema hali Ghaza, kijumla, ni ya kushtusha kabisa

Christopher Gunnes, Msemaji wa Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA), ameiambia Redio ya UM-Geneva, kwamba hali katika Tarafa ya Ghaza ni mbaya sana, na kila saa masaibu na maafa ya kiutu yanaendelea kukithiri. Alisema watu milioni moja

Mashambulio ya majengo ya UM Ghaza lazima yachunguzwe na tume huru, UNRWA yasisitiza

Kadhalika Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA), limesema linataka kufanyike uchunguzi halali, ulio huru, kuhusu mashambulio ya majengo ya UNRWA yaliotoa hifadhi kwa watu waliokimbia mapigano, katika Jabaliya, ambapo watu 40 ziada waliuawa wiki hii.

ICRC yashtumu Israel kwa kukiuka kanuni za kimataifa kuhusu majeruhi wa mapigano.

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) imeripoti leo, kwa kupitia msemaji wake Geneva, Dominik Stillhart, kwamba majeshi ya Israel “yameshindwa kutekeleza majukumu yao, chini ya sheria za kiutu za kimataifa za kuhudumia majeruhi wa vita.”

WHO inasema huduma za afya Ghaza zimevurugika

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti huduma za afya ya jamii katika Tarafa ya Ghaza zinahitajia, kidharura vifaa, madawa na wafanyakazi.