Wanawake

Vikosi vya Rwanda vyaruhusiwa na serikali ya JKK kuwasaka waasi wa FDLR

Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC) limetangaza rasmi kwamba wanajeshi karibu 2,000 wa Rwanda Ijumanne waliruhusiwa kuingia katika JKK, kwa kupitia eneo la mashariki, kuwasaka waasi wa Rwanda, wa kundi la FDLR, wenye asili ya kiHutu ambao inaripotiwa ndio miongoni mwa makundi yenye kupalilia hali ya wasiwasi kieneo kwa muda wa zaidi ya miaka kumi.

Mukhtasari wa shughuli katika BU

Baraza la Usalama leo asubui linazingatia Operesheni za Kulinda Amani za UM katika Cote d’Ivoire pamoja na Ripoti ya KM juu ya suala hilo.

Mkurugenzi wa UNRWA athibitisha huduma za afya zimefufuliwa Ghaza kufuatia mapigano

Dktr Guido Sabatinelli, Mkurugenzi wa Afya wa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kiutu kwa Wahamiaji wa KiFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA), kwenye mazungumzo na waandishi habari mjini Geneva alielezea juu ya hali dhaifu iliokabili sekta ya afya, ambayo imeharibika zaidi kutokana na mashambulio ya wiki tatu zilizopita.

Wahamaji wa IDPs Sudan wahitajia huduma za dharura za maji

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limechapisha ripoti yenye kuonyesha wahamaji wa ndani ya nchi (IDPs), katika Sudan Kusini na Korodofan ya Kusini sasa hivi hukabiliwa na matatizo makubwa ya maji, pale wanaporejea makwao kutoka kambi za makazi ya muda.

Kipindupindu kinaendelea kupamba Zimbabwe licha ya mchango wa kimataifa

Shirika la IOM limeeleza kwamba katika kipindi cha kuanzia tarehe 20 Disemba 2008 hadi 10 Januari 2009 lilifanikiwa kuwafikia watu 160,000 na kuwapatia tembe za kusafisha maji na nasaha kinga dhidi ya maradhi ya kipindupindu katika maeneo ya Zimbabwe ya Harare, Bulawayo na Mutare.

KM aihimiza Israel kuondosha vikosi Ghaza na kunasiihi WaFalastina kukomesha hujuma za makombora ya kienyeji

KM Ban Ki-moon alibainisha matumaini yake Ijumapili ya kuwa usmamishaji wa upande mmoja wa mashambulizi ya Israel, ya siku 22 dhidi ya eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza humaanisha matumaini mema kwenye juhudi za kudumisha amani kieneo.

Msemaji wa UNRWA akiri hali shwari Ghaza lakini bado ni ya wasiwasi

Chris Gunness, Msemaji wa Shirika la UM Linalofarajia Misaada ya Kihali kwa WaFalastina wa Mashariki ya Karibu (UNRWA) alihojiwa Ijumatatu, kwa kupitia njia ya simu, na Idhaa ya Redio ya UM-Geneva ambapo alielezea namna hali ilivyo sasa hivi katika Ghaza, baada ya kutangazwa vikosi vya Israel vinasimamisha mashambulizi:~

UNAMID inaahidi itaendelea kuhami raia Darfur Kusini, licha ya kufumka kwa mapigano

Minni Minawi, Ofisa Msaidizi wa Raisi na Kongozi wa jeshi la mgambo la Sudan la SLA/MM Ijumapili alizuru Makao Makuu ya Vikosi vya Amani vya Mchanganyiko vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID) katika mji wa El Fasher na kukutana, kwa mashauriano, na Naibu Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UNAMID [Henry Anyidoho] na vile vile maofisa wa ngazi za juu wengine kuzingatia hali ya usalama katika mji wa Muhajeriya, Darfur Kusini .. ambapo katika siku za karibuni mapigano makali yalishuhudiwa huko baina ya kundi la JEM na SLA/MM.

UNICEF inasema wajawazito wa mataifa yanayoendelea hukabiliwa na hatari ya vifo vya uzazi kwa wingi zaidi kushinda nchi tajiri

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) hii leo limewasilisha ripoti mpya ya mwaka kuhusu “Hali ya Watoto Duniani”.

Baraza la Haki za Binadamu laandaa tume ya kuchunguza ukiukaji wa haki katika Ghaza

Raisi wa Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu, naye anajiandaa pia kutayarisha mazungumzo ya dharura ya kuteua wajumbe wa tume maalumu ya uchunguzi, itakayopelekwa Ghaza kuthibitisha yale madai ya kwamba majeshi ya Israel yamekiuka haki za binadamu kutokana na opereshenzi zao kwenye eneo husika.