Nchini Uganda, wakimbizi katika makazi yao ya Kyangwali mjini Hoima, wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa maandamano, shughuli za kitamaduni huku vyote vikimulika umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika juhudi za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi sambamba na athari za mabadiliko hayo kwao hasa wakimbizi nchini Uganda.