Muungano wa Afrika AU na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO wamesema wanaimarisha ushirikiano wao ili kuhakikisha uchumi wa kilimo barani Afrika unaleta tija kwa mamilioni ya watu wa bara hilo.
Katika visiwa vya Pacifiki kati ya asilimia 75 hadi 90 ya wachuuzi sokoni ni wanawake na kwa kutambua umuhimu wao na mchango wao katika jamii shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women liliamua kuanzisha mradi wa masoko kwa kwa ajili ya mabadiliko au M4C kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hao na familia zao.
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa kwa ajili ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana, Umoja wa Mataifa umesema umedhamiria kukomesha mifumo yote ya ukatili kwa kundi hilo kwani ni wajibu na haki kufanya hivyo.
Mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto CRC ambao mwaka huu umetimiza miaka 30 tangu upitishwe na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unataja bayana haki kuu nne za msingi ambazo kile mtoto, yaani mkazi wa dunia mwenye umri wa miaka 18 au chini ya hapo anapaswa kuzipata awe wa kike au wa kiume.
Pamoja na kukabiliwa na ubaguzi na unyanyasaji wa kingono, wanawake nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR, wamechukua hatua ya kuwapatia matumaini wenzao wanaorejea katika makazi yao walimofurushwa kutoka na mapigano katika jamii zao.
Miaka 25 ilityopita dunia iliweka ahadi ya kuhakikisha afya ya uzazi kwa wanawake na wasicha inakuwa ni haki ya msingi ili kuwawezesha kuwa huru na kufanya maamuzi ya maisha yao. Sasa umewadia wakati wa kutimiza ahadi hiyo kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa shirika la idadi ya watu duniani UNFPA, Dkt. Natalia Kanem.
Meja Seynabou Diouf kutoka jeshi la polisi la taifa la Senegal amechaguliwa na kutangazwa kutwaa tuzo ya polisi mwanamke wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2019.
Dhamira yetu kubwa kama chama cha wandishi wa habari wanawake, TAMWA visiwani Zanzibar nchini Tanzania ni kuwatetea wanawake na watoto kwa kupaza sauti zao kupitia vyombo vya habari.