Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea kutiwa moyo na hatua ya mamlaka Thailand kuruhusu Rahaf Mohammed Al-qunun kutoka kwenye hoteli ilioko kwenye uwanja wa ndege, Bangkok na kwamba UNHCR iliruhusiwa kuonana naye na kwa sasa yupo maeneo salama mjini humo.