Ukatili wa kijinsia na usafirishaji haramu wa binadamu vimekuwa donda ndugu nchini Somalia, sasa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM lmeamua kuvalia njuga changamoto hizo.
Redio za kijamii zina mchango mkubwa katika kumuendeleza mwanamke wa kijijini. Hiyo ni moja ya kauli zilizotanabaishwa wakati wa mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW uliomalizika hivi karibuni jijini New York, Marekani.
"Baada ya kupata mafunzo ya usindikaji bidhaa, nimeona mafanikio makubwa sana katika kilimo na biashara na pia bidhaa zetu zinadumu muda mrefu bila kuharibika".
Watu bilioni 1.7 wanaishi vijijini kote duniani huku zaidi ya asilimia 40 ya nguvu kazi yao katika kilimo ni wanawake ambao wakiilisha na kuindeleza jamii lakini wanasalia kuwa ndio masikini wakubwa.
Takwimu ni muhimu sana ili kuonyesha ni kwa kiasi gani mwanamke wa kijijini anachangia katika uzalishaji na maendeleo hasa katika vita vya ukombozi wake.
Bila msaada wa kibinadamu maisha ya raia wengi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yako mashakani. Onyo hilo limetolewa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaehusika na masuala ya kuratibu misaada ya kibinadamu , Mark Lowcock wakati akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo na kuelezea hali ilivyo DRC.
Wakati mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW62 ukiendelea jijini New York, Marekani wawakilishi wa mashirika ya kiraia kutoka Tanzania wamezungumziaumuhimu wa suala la uwezeshaji wanawake vijijini kupitia mafunzo mbalimbali waliyoyapata kwenye mkutano huu.