Wanawake

UNFPA yaomba msaada wa dola mil 10.7 kusaidia wanawake na wasichana wa Sri Lanka

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA, limetoa ombi la dola milioni 10.7 kwa ajili ya kutoa usaidizi wa kuokoa maisha kwa wanawake na wasichana zaidi ya milioni mbili nchini Sri Lanka. 

Shule ya Kakenya Dream yazidisha mapambano dhidi ya mila potofu kwa jamii za kimasai

Kenya ni moja ya nchi za kwanza barani Afrika kuridhia mkataba wa kulinda haki za watoto wa Umoja wa mataifa. Ijapokuwa hatua zimepigwa kuimarisha hali ya watoto bado kazi ipo zaidi inayohitaji kufanywa na jamii kwa ujula ili kulinda maslahi ya watoto.

UNFPA yatangaza washindi 10 wa miradi ya kuwawezesha wanawake na wasichana

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA, leo limetaja washindi 10 wa pamoja wa shindano la miradi bunifu inayoweza kuleta mabadiliko chanya na kuwezesha wanawake na wasichana duniani. 

Kesi za unyanyasaji kingono zaongezeka kwa asilimia 218 nchini Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS umeeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kutokan na kuongezeka kwa kesi za unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro zinazoibuka licha ya kupungua kwa jumla kwa idadi ya raia walioathiriwa na ghasia nchini humo.

Takriban nusu ya watoto wenye UKIMWI hawapati matibabu

Wakati zaidi ya robo tatu ya watu wazima wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI VVU wanapata aina fulani ya matibabu, idadi ya watoto wanaofanya hivyo, inafikia asilimia 52 pekee. 

Taliban endeleeni kushughulikia kuhusu haki za binadamu nchini Afghanistan: UNAMA

Baada ya mamlaka ya Taliban kuwepo madarakani kwa zaidi ya miezi 10 sasa, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umetoa ripoti yake kuhusu haki za binadamu na masuala mengine nchini humo.

Viongozi wa Afrika wazindua mpango wa ‘Eduation Plus’ kusaidia wasichana kuendelea na shule 

Viongozi waliokutana katika mkutano wa Muungano wa Afrika mjini Lusaka, Zambia hii leo wameahidi kuunga mkono mpango wa ‘Education Plus’ wakijitolea kuchukua hatua ya kuwafanya wasichana kubaki shuleni, jambo ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wao wa kuambukizwa Virusi Vya UKIMWI, VVU. 

Wanawake kwenye sekta ya Afya wanalipwa 24% pungufu ya wenzao wa kiume

Wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya afya na huduma wanalipwa ujira mdogo zaidi kuliko sekta nyingine za kiuchumi na wanalipwa asilimia 24 pungufu ya wenzao wa kiume hata pale wanapokuwa na vigezo sawa katika soko la ajira. 

UNMISS yaendesha mafunzo ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha mafunzo ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji katika eneo la makutano la  Aru jimboni Equatoria ya Kati ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaandaa wananchi kujilinda kwa kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekuwa vikijirudia na kuathiri zaidi wanawake na wasichana. 

Karibu theluthi ya wanawake wote katika nchi zinazoendelea wanajifungua wangali vigori:UNFPA

Matokeo ya utafiti mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani na masuala ya afya ya uzazi UNFPA yaliyotolewa leo yanaonesha kuwa karibu theluthi moja ya wanawake wote katika nchi zinazoendelea wanaanza kupata Watoto wakiwa na umri wa miaka 19 au chini ya hapo, na karibu nusu ya uzazi wote wa mara ya kwanza wa barubaru huwa ni wa Watoto au wasichana wa umri wa miaka 17 au chini ya hapo.