Wanawake

WHO imezindua mtandao wa kimataifa wa miji kuwaenzi vikongwe

Shirika la afya duniani WHO leo limezindua mtandao wa kimataifa wa miji kuthamini wazee kama sehemu ya kwenda sambamba na ongezeko la idadi ya vikongwe.

Israel imeaswa kuepuka ukiukaji zaidi wa haki mashariki mwa Jerusalem

Mwakilishi maalimu wa Umoja wa Mataifa Richard Falk ameitaka Israel kuzuia ukiukaji zaidi wa sheria za kimataifa Mashariki mwa Jerusalem.

Msaada wa haraka wa dawa unahitajika nchini Kyrgystan:OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kuratibu masuala ya kibinadamu OCHa imesema kuna haja ya haraka ya kupatikana dawa nchini Kyrgystan.

Kura za Urais zinaendelea kuhesabiwa Burundi kukiwa na hofu ya usalama

Kura za uchaguzi wa Rais zinaendelea kuhesabiwa nchini Burundi huku kukiwa na wasiwasi baada ya jana usiku kutokea milipuko ya guruneti katika eneo lenye watu wengi.

UM unaitaka Jamhuri ya Afrika ya Kati kuendelea na maandalizi ya uchaguzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka pande zote nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuendelea na maandalizi ya uchaguzi wa Rais na wabunge.

UM umepongeza kura ya maoni kufanyika kwa amani na utulivu Kyrgystan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mwakilishi wake nchini Kyrgyzstan wamekaribisha kura ya amani ya katiba iliyofanyika jana.

Ban amelaani shambulio dhidi ya kituo cha michezo cha UNRWA Gaza

Watu mbalimbali wamekuwa wakitoa kauli kufuatia shambulio la leo asubuhi Gaza dhidi ya kituo cha michezo ya kiangazi cha UNRWA.

Wakimbizi wa Rwanda wahofia kurejea nyumbani yasema UNHCR

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa nchini Uganda inasema wakimbizi wa Rwanda wanahofi kurejea nyumbani.

UM umelaani shambulio lingine dhidi ya kituo cha michezo cha UNRWA

Mkuu wa uperesheni za misaada wa Umoja wa Mataifa Gaza amelaani shambulio la leo asubuhi katika moja ya vituo vya michezo vinavyotumiwa na watoto katika eneo hilo.

Wananchi wa Burundi leo wamepiga kura katika uchaguzi wa Rais

Wananchi wa Burundi leo wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais kukiwa na mgombea mmoja pekee katika kiti hicho.