Wanawake

Mapigano ya karibuni Mogadisho yawaong'olesha makazi 200,000 ziada, imeripoti UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti, kwa kupitia msemaji wake aliopo Geneva, kwamba muongezeko wa mapigano yaliovuma karibuni kwenye mji wa Usomali, wa Mogadishu, ni hali iliozusha athari mbaya kabisa kwa wakazi waliolazimika kuhama mastakimu yao, na kuleta usumbufu mkubwa kwa raia wa kawaida.

Mjumbe Maalumu wa Maziwa Makuu hakuridhika na maendeleo ya kurudisha amani

Mjumbe Maalumu wa UM juu ya Masuala ya Maziwa Makuu, Olusegun Obasanjoaliyekuwa raisi wa zamani wa Nigeria, ambaye anazuru Mako Makuu kushauriana na wakuu wa UM kuhusu hali ya eneo, aliwaambia waandishi habari Ijumanne kwamba maendeleo ya kurudisha utulivu na amani katika eneo la vurugu, la mashariki katika JKK yanajikokota, hasa kwenye zile juhudi za kukomesha uhasama baina ya makundi ya waasi na vikosi vya Serikali.

Chanjo ya TB kwa watoto wachanga wenye VVU inadhuru, kuonya wataalamu Afrika Kusini

Uchunguzi wa wataalamu wa Afrika Kusini, ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la afya la Shirika la Afya Duniani (WHO) umethibitisha kwamba ile chanjo kinga dhidi ya kifua kikuu (TB), ambayo kikawaida hupewa asilimia 75 ya watoto wachanga ulimwenguni, baada ya kuzaliwa, inakhofiwa dawa hii huleta madhara kwa watoto walioambukizwa na virusi vya UKIMWI na husababisha hata vifo.

Wahisani wahimizwa na UNCTAD kutekeleza ahadi za kuimarisha kilimo Afrika

Kwenye kikao cha Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) kilichofanyika Ijumanne Geneva kuzingatia mzozo wa chakula katika Afrika, wahisani wa kimataifa walihimizwa kutekeleza haraka ahadi walizotoa siku za nyuma kuimarisha kilimo bora barani humo.