Wanawake

ICTR imehukumu kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki Rwanda

Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) leo imemhukumu Tharcisse Renzaho, aliyekuwa kiranja wa Kigali-ville na pia Kanali wa Jeshi la Rwanda katika 1994, adhabu ya kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya halaiki, makosa ya vita na uhalifu dhidi ya utu.

Amani ya chakula ndio msingi wa usalama wa dunia:IFAD

Kanayo Nwanze, Raisi wa Taasisi ya UM juu ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwenye mahojiano aliofanya na Redio ya UM alisisitiza juu ya umuhimu wa ile rai ya walimwengu kuhakikisha kunakuwepo akiba maridhawa ya chakula duniani.

UNHCR ina wasiwasi juu ya madai wanamaji wa Utaliana waliwatendea kusio huruma wahamiaji wa Eritrea

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ameripoti leo hii, kutokea Geneva, ya kuwa watumishi wa UNHCR waliopo Libya, walifanikiwa kufanya mahojiano na watu 82 waliozuiliwa karibuni na manowari za Utaliana, kwenye eneo la bahari kuu liliopo maili za bahari 30 kutoka kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa.

Uwezo wa kufanyiza dawa ya chanjo dhidi ya A(H1N1) ni mdogo, ahadharisha mkuu wa WHO

Imeripotiwa na UM kwamba uwezo uliopo sasa wa kutengeneza chanjo kinga dhidi ya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1) ni mdogo na hautoweza kukidhi mahitaji ya watu bilioni 6.8 waliopo ulimwenguni sasa hivi, idadi ambayo inakabiliwa na uwezo wa kuambukizwa kirahisi na kuathirika na virusi vipya hatari vya homa hiyo.

Hapa na pale

Ad Melkert, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Iraq ameripoti kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulio ya karibuni nchini, ambapo Wakristo walio wachache walihujumiwa pamoja na taasisi zao za kidini na makundi yasiotambulikana. Alieleza hisia hizo baada ya makanisa kadha kushambuliwa Ijumapili katika miji ya Baghdad na Mosul, mashambulio yaliosababisha vifo vya watu wanne na darzeni za majeruhi. Melkert alisema "kampeni hii ya vurugu imekusudiwa kupalilia vitisho miongoni mwa makundi yalio dhaifu, na kwa lengo la kuzuia watu wa dini tofauti kuishi pamoja kwa amani, kwenye moja ya eneo maarufu miongoni mwa chimbuko kuu la kimataifa lenye kujumlisha anuwai za kidini na kikabila. Melkert alitoa mwito uyatakayo makundi husika yote, ikijumlisha Serikali ya Iraq, kuongeza mara mbili zaidi jitihadi zao za kuwapatia wazalendo walio wachache ndani ya nchi, hifadhi kinga na kuimarisha anuwai ya kidini, kikabila na kitamaduni iliopo katika Iraq kwa karne kadha wa kadha.

Kesi ya Charles Taylor yaanza rasmi Hague

Mawakili wa utetezi wa mtuhumiwa Charles Taylor, aliyekuwa raisi wa Liberia, wameanza kumtetetea mshitakiwa hii leo mjini Hague, Uholanzi kwa kusisitiza mtuhumiwa hajahusika na mauaji yalioendelezwa na waasi wa Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshtadi nchini mika ya nyuma, na wala hajahusika na vitendo vya kujamii kimabavu raia au kulemaza watu wasio hatia.

Mashirika ya UM kuanzisha Kituo cha Isange kuhudumia waathirika wa mabavu Rwanda

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Wanawake (UNIFEM) limeripoti kutiwa sahihi maafikiano ya pamoja, kati ya mashirika ya UM na Serikali ya Rwanda, ya kuanzisha kituo maalumu cha kuwahudumia kihali na kiakili wale wanawake na watoto wanaoteswa na vitendo vya kutumia nguvu na mabavu dhidi yao.

Vikosi vya Serikali Usomali vyapatiwa msaada ziada wa walinzi amani wa UA dhidi ya wapiganaji wapinzani

Kadhalika, imeripotiwa walinzi amani wa Umoja wa Afrika waliopo Mogadishu, waliingilia kati, kwa mara ya kwanza, moja kwa moja, mapigano kwa madhumuni ya kuvisaidia vikosi vya Serikali kupambana na makundi ya wapinzani.

Mjumbe Maalum wa KM kwa Usomali ana matumaini utulivu utarejeshwa nchini karibuni

Wiki iliopita Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, Antonio Guterres, alibainisha kwamba tangu mapigano kufumka katika mji wa Mogadishu, mnamo mwanzo wa mwezi Mei, baina ya vikosi vya Serikali na makundi ya upinzani yaliojumuisha majeshi ya mgambo ya Al-Shabab na Hizb-al-Islam, watu 200,000 inaripotiwa walilazimika kuhajiri makazi, kiwango cha uhamaji ambacho kilishuhudiwa kieneo mara ya mwisho katika mwaka 2007, pale vikosi vya Ethiopia vilipoingilia kati, kwa nguvu, mgogoro wa Usomali.

Viongozi wa G-8 wameahidi msaada wa kilimo wa $20 bilioni kwa nchi masikini

Viongozi wa Kundi la G-8 waliokutana kwenye mji wa L\'Aquila, Utaliana kabla ya kuhitimisha kikao chao waliahidi kuchangisha dola bilioni 20 za kuzisaidia nchi masikini kuhudumia kilimo, ili waweze kujitegemee chakula kitaifa badala ya kutegemea misaada ya kutoka nchi za kigeni, hali ambayo ikidumishwa itasaidia kukomesha duru la umaskini na hali duni.