Wanawake

UNHCR inasailia majaaliwa ya wahamiaji wa Kisomali katika Kenya

Mapema wiki hii Shirika la UNHCR liliripoti wasiwasi wake kuhusu taarifa ilizopokea zilizothibitisha kwamba Serikali ya Kenya huwarejesha makwao kwa nguvu makwao,wale wahamiaji wa Kisomali wenye kuomba hifadhi ya kisiasa.

Hatua ziada zahitajika kudhibiti kipindupindu Zimbabwe, inasema WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa mwito muhimu wa kutaka kuchukuliwa hatua ziada, za haraka, kudhibiti kipindupindu nchini Zimbabwe, maradhi ambayo bado yanaendelea kutesa raia kwa kasi kuu.

UM inakhofia usalama wa raia kufuatia operesheni za majeshi ya Rwanda/JKK dhidi ya FDLR

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM Linalohudumia Wahamiaji (UNHCR) ameripoti kutoka Geneva kwamba hali ya wasiwasi imeanza kutanda tena kwenye jimbo la Kivu kusini, katika JKK kufuatia operesheni za pamoja za karibuni za majeshi ya Rwanda/JKK dhidi ya waasi wa wanamgambo wa kundi la FDLR.

Waasi wa LRA walihusika na mauaji ya raia katika JKK, OCHA imethibitisha

Vile vile kuhusu JKK, Elizabeth Byrs, Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ametoa taarifa yenye kuthibitisha ya kuwa baina ya tarehe 1 hadi 20, Januari mwaka huu, waasi wa Uganda wa kundi la LRA waliosakama katika JKK, walishambulia mitaa 19 katika wilaya ya Haut Uele, kwenye jimbo la Orientale na kuua raia 269, na baadaye kufanya uharibifu wa mali, na kuiba pamoja na kuchoma moto nyumba za raia.

KM ahimiza mchango ziada wa mataifa tajiri kuimarisha maendeleo ya nchi maskini

Kwenye mkutano na waandishi habari uliofanyika Davos, Uswiss, KM Ban Ki-moon alitoa mwito maalumu wenye kusihi mataifa matajiri kutowasahau wanadamu wenziwao katika nchi maskini, hasa katika kipindi ambacho maendeleo ya uchumi yamepwelewa na yanaendelea kuporomoka duniani.

Wapiganaji waasi wa Rwanda waliopo JKK wapatiwe fursa ya kurudi makwao, bila kulazimishwa, inasema UM

Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) ameripotiwa akisema kwamba rai ya kuruhusu Wanyarwanda waliokuwa wakipigana na majeshi ya mgambo nchini Kongo kuzuru makwao na kuchunguza kama hali inafaa kwao kurejea, ni moja ya taratibu ambazo zikitekelezwa kama inavyopasa, zitasaidia kupunguza vurugu na uhasama unaofufuka mara kwa mara kwenye eneo la uhasama Kongo. Mradi huo, alisisitiza Doss, unabashiria “mapatano mema kati ya Serikali za Rwanda na JKK, yalioamua hatua za kuchukuliwa, zilizo salama,” za kuwarejesha makwao wale wapiganaji waliotokea Rwanda ikiwa wapiganaji hawo wataridhia kurejea kwa hiyari.

Benki maarufu Afrika yaafikiana na UM kupiga vita pamoja maradhi maututi

Benki muhimu maarufu inayohudumia Afrika ya Standard Bank, Ijumatatu imetiliana sahihi na Taasisi ya Mfuko wa Kimataifa Dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria – inayoungwa mkono na UM – yaani Taasisi ya Global Fund, makubaliano ya kutoa huduma, bila malipo, za kusimamia matumizi ya misaada ya kupambana na majanga hayo matatu ya maradhi maututi wanayopokea mataifa husika katika Afrika.

UNFPA kuipongeza serikali mpya Marekani kwa kuchangisha tena misaada kwa Shirika

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu UNFPA) limepongeza uamuzi wa Raisi Barack Obama wa Marekani kuanza tena kutoa mchango wa taifa lake, kufadhilia operesheni za UNFPA za kupunguza ufukara, kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuimarisha uzazi bora kwa mama wazazi katika mataifa 154 ulimwenguni. ~ ~

UNICEF/WHO kufadhiliwa dola milioni 9.7 na Waqf wa Gates kuhudumia watoto dawa bora

Taarifa iliotolewa bia leo hii na mashirika mawili ya UM yanayohudumia maendeleo ya watoto, yaani UNICEF, na afya duniani, yaani WHO, imepongeza msaada wa dola milioni 9.7 waliopokea kutoka Waqf wa Bill na Melinda Gates, kwa makusudio ya kuimarisha utafiti wa kutengeneza dawa zitakazotumiwa makhsusi, na kwa urahisi, na watoto wadogo chini ya umri wa miaka kumi na tano.

Wajumbe wa kimataifa wakutana Roma kuandaa miradi ya kudhibiti bora maji duniani

Wajumbe wa kimataifa kutoka nchi 60 ziada wanakutana mjini Roma, Utaliana kwenye Makao Makuu ya Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) kuanzia leo tarehe 21 mpaka 23 Januari (2009) ambapo wataendelea kujadiliana mpango wa utendaji, unaohitajika kudhibiti bora matumizi ya maji ulimwenguni, kufuatia athari mbaya za mazingira zinazochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.