Wanawake

UNHCR unatoa wito wa msaada kwa wakimbizi jamhuri ya Kongo

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetangaza wito wa dharura wa msaada ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi laki moja na saba huko Jamhuri ya Kongo walokimbia ghasia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ban anahisi kuna changamoto kabla ya kukamilika amani Sudan

Mwaka huu wa mwisho wa utekelezaji wa makubaliano ya amani ya 2005 yaliyotiwa saini kati ya kundi la ukombozi wa Sudan SPLA na serikali ya Sudan, utakua mgumu sana, amesema katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon.

Mradi vijiji vya millenia wapongeza kwa vita dhidi ya HIV/Ukimwi

Mshauri wa juu wa katibu mkuu amepongeza juhudi za mradi wa Vijiji wa Milenia MVP wa UNAIDS katika vita vya kupambana na ukimwi.

OCHA yasema Umoja wa Mataifa hauna mpango wa kuitelekeza Somalia

Umoja wa mataifa hauna mpango wa kuitelekeza Somalia licha ya mazingira magumu yanayoambatana na vitisho na ghasia wanayokabiliana nayo wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu.

ICRC yasaidia kuachiliwa huru askari sita Congo DRC

Katika operesheni mbili tofauti zilizofanyika jana na leo kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu (ICRC) imesaidia katika kuachiliwa na kusafirishwa kwa wanajeshi sita wa jeshi la Congo waliokuwa wanashikiliwa na makundi yenye silaha katika majimbo ya Kivu ya Kusini na Kaskazini.

Watu 130 wauawa na wapiganaji wa kijadi wakati hofu ikiongezeka Sudan Kusini

Wapiganaji wa kijadi wenye silaha wa kabila la Nuer wamewaua takribani watu 139 kutoka kabila hasimu wao, katika kijiji kimoja kusini mwa Sudan, amesema afisa mmoja wa serikali hii leo.

Masharika ya misaada yataka dunia kuchukua hatua kuzuia vita mpya Sudan

Vita kubwa huenda ikarejea Sudan Kusini iwapo dunia haitachukua hatua ya kulinda mkataba wa amani ambao ulimaliza moja ya vita kubwa na ya muda mrefu barani Afrika.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imetakiwa kulishughulikia suala la kuwalinda watoto katika vita

Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto Walionaswa kwenye Mapigano. Bi Radhika Coomaraswamy, ameitaka mahakama ya kimataifa ya uhalifu kushughulikia suala la jinsi ya kuwalinda watoto wanaojihusisha kwa njia mbalimbali katika vita.

Kongaano la Umoja wa Mataifa lanuia kwarejesha pamoja raia wa Chad

Leo Januari sita Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP), kwa mara ya kwanza limewakutanisha pamoja jamii, viongozi wa dini, na viongozi wa kijeshi ili kubaini ni kwa njia gani jamii zilizosalia na makovu ya vita zinaweza kuishi pamoja kwa amani mashariki mwa Chad.

Ushahidi dhidi ya Thomas Lubanga kutolewa na mjumbe wa UN

Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Watoto Walionaswa kwenye Mapigano atatoa ushahidi mbele ya Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) dhidi ya Thomas Lubanga.