Wanawake

UM una wasiwasi mkubwa kutokana na vizuizi dhidi ya Gaza

Umoja wa Mataifa ulieleza Ijumatano kwamba ina wasi wasi mkubwa kutokana na kuzorota mfumo wa huduma ya afya kwenye ukanda wa Gaza kutokana na Israel kufunga mipaka ya eneo hilo linalotawaliwa na Hamas.

Mkurugenzi Mkuu wa WFP atatembea Haiti

Mkurugenzi mkuu wa idara ya chakula duniani WFP, Josette Sheeran anatarajiwa kuwasili Haiti Alhamisi kutathmini binafsi hali ilivyo kufuatia maafa kutokana na tetemeko la ardhi la wiki iliyopita.

IOM kuimarisha juhudi baada ya kufahamu haja walopeteza makazi yao Haiti

Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM limesema litaweza kuwapatia hadi wathiriwa elfu 25 wa tetemeko la ardhi katika mji mkuu wa Port-au-prince msaada usio wa chakula, linapoimarisha misaada yake katika maeneo matano ya mji mkuu huko Haiti.

Benki Kuu kutoa msaada zaidi wa dola milioni 100 kwa Haiti

Benki Kuu ya Dunia itatoa msaada zaidi wa dola milioni 100 kama mkopo wa dharura kusaidia kazi za uwokozi na kuikarabati taifa la Caribbean la Haiti.

Haiti yakumbwa na tetemeko jingine

Haiti imekumbwa tena na tetemeko kubwa Ijumatano, na kutikisa majengo na kusababisha mtaharuku mkubwa, watu wakikimbia barabarani baada ya kushuhudia mtetemeko mkubwa ulosababisha maafa siku nane zilizopita.

Mashirika yafanya maendeleo kuwafikia wathiriwa Haiti

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaripoti kwamba wanafanya maendeleo makubwa katika kufikisha msaada wa dharura unaohitajika sana na maelfu ya walonusurika tetemeko la ardhi huko Haiti.

UNHCR:Wasomali elfu 60 wakimbia makazi yao

Idadi ya majeruhi wa ki-somali na wale wanaopoteza makazi yao inaongezeka kutokana na kuendelea kwa mapigano katika wilaya za kati za Somalia.

Pakistan yazuia ajenda kwenye mkutano wa kupunguza silaha

Majadiliano juu ya kupunguza silaha za nukilia duniani hayakuweza kuanza Ijumanne wakati Pakistan ilipozuia kuidhinishwa kwa ratiba ya 2010 ya mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya kupunguza silaha huko Geneva.

Lazima UM kuendelea na jukumu la mazungumzo ya hali ya hewa

Mkurugenzi mkuu wa Idara ya mazingira ya UM Achim Steiner anasema ni lazima kwa majadiliano ya kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani yabaki chini ya uwongozi wa UM hata ikiwa mkutano wa viongozi wa Copenhagen mwezi Disemba haukufanikiwa kuleta ufumbuzi.

UNHCR: Idadi ya waafrika wanaokimbia kutoka pembe ya Afrika imeongezeka kwa 55%

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), iliwapokea watu wepya elfu 77 802 kutoka Pembe ya Afrika mwaka 2009 ikiwa ni muongezeko wa asili mia 55 kulingana na mwaka 2008 na mara ya kwanza wa-Somali hawakua wengi kuliko watu wa mataifa mengine alieleza afisa wa uhusiano wa mambo ya kigeni wa idara hiyo Rocco Nuri.