Wanawake

Bodi la Utawala UNCTAD kutathminia ufufuaji wa kilimo Afrika

Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD) linatarajiwa Ijumanne jioni kukutana Geneva, kufanya tathmini kuhusu juhudi za kufufua kilimo katika bara la Afrika, huduma ambazo zimezorota katikati ya kipindi kilichopambwa na athari haribifu zilizoletwa na mizozo ya uchumi dhaifu kwenye soko la kimataifa.

Wajumbe wa Kundi la Kazi la UM kwa waliopotezwa na kutoweka wahitimisha kikao cha 88 Rabat

Wajumbe wa Kundi la Kufanya Kazi la UM juu ya Watu Waliolazimishwa Kupotea na Kutoweka baada ya kukukamilisha ziara yao ya siku nne katika Morocco walikutana kwenye mji wa Rabat na kukamilisha kikao cha 88 kilichofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Juni walipozingatia masuala yanayohusika na watu kukamatwa kimabavu na kutoweka wasijulikane walipo.

ICRC inasema miezi sita baada ya mashambulio ya Israel Ghaza inaendelea kusumbuka na kuteseka kimaisha

Ripoti mpya ya Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) iliotangazwa hii leo, inaeleza ya kuwa umma wa eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza, unaendelea kusumbuka na kuteseka kimaisha, miezi sita baada ya operesheni za kijeshi za Israel kuendelezwa dhidi ya eneo hili la Mashariki ya Kati.

WHO-UNICEF yasisitiza jitihadi kuu zahitajika kuhifadhi mahospitali na skuli penye maafa

Mashirika ya UM juu ya afya na maendeleo ya watoto, yaani mashirika ya WHO na UNICEF, yametoa mwito wa pamoja wenye kuzihimiza serikali za kimataifa, kuchukua hatua madhubuti, katika sehemu nne muhimu zinazohitajika kupunguza athari za maafa katika mahospitali na maskuli.

Siku ya Kimataifa kwa Mtoto wa Afrika

Tarehe ya leo, Juni 16, inaadhimishwa na UM kuwa ni "Siku ya Kimataifa kwa Mtoto wa Afrika." Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza ya kuwa kuna baadhi ya nchi katika Afrika, zilizoonyesha maendeleo makubwa ya kutia moyo, kwenye zile juhudi za kuhudumia watoto wachanga kuishi.

IAEA inaripoti matumaini kuhusu mazungumzo ya Iran-Marekani, na wasiwasi kufuatia majaribio ya kinyuklia ya DPRK

Ripoti ya Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Kinyuklia (IAEA), Mohamed ElBaradei iliowakilishwa kwenye Bodi la Magavana, imebainisha kuwa na matumaini ya kutia moyo, katika kuanzisha mazungumzo baina ya Teheran na Washington, kuzingatia masuala ya miradi ya kinyuklia inayoendelezwa na Iran hivi sasa pamoja na mada nyeginezo.

Nusu ya vifo vya barabarani huathiri wenda kwa miguu, wapanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki

Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) umethibitisha ya kuwa nusu ya watu milioni 1.27 wanaokadiriwa kufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, ni watu wanaokwenda kwa miguu, na wale wanaopanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki.

Ulimwengu sasa umo kwenye mkumbo wa awali wa maambukizo ya janga la homa ya A(H1N1), yahadharisha WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki hii limepandisha kiwango cha tahadhari ya maambukizi ya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1) kutoka daraja ya 5 mpaka ya sita.

Siku ya Dunia Dhidi ya Ajira ya Watoto Wadogo

Kwenye kumbukumbu ya miaka 10 ya Siku ya Dunia dhidi ya Ajira ya Watoto wa Umri Mdogo, siku ambayo huadhimishwa tarehe ya leo kulitolewa mwito maalumu na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), likijumuika na mashirika wenzi wa kuhimiza jamii ya kimataifa kukabiliana na sababu za msingi zenye kuchochea umasikini na ufukara, hali ambayo inaaminika ndio yenye kuwalazimisha watoto wenye umri mdogo kutafuta ajira ya kumudu maisha.

Mapigano Usomali yazusha msururu was maafa, mamia ya majeruhi na uhamisho wa lazima

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mapigano makali yalioshtadi katika mji mkuu wa Mogadishu, Usomali mnamo miezi ya karibuni, yamewacha nyuma msururu wa uharibifu na maangamizi, majeruhi kadha wa kiraia na kusababisha mamia elfu ya watu kulazimika kuhama makazi na kuelekea maeneo tofauti ya nchi yenye hifadhi bora.