Kwa mara ya kwanza, Umoja wa Mataifa unaadhimhisha hii leo siku ya mabunge duniani, ikiwa ni siku pia ambayo Umoja wa Mabunge duniani, IPU ulianzishwa mwaka 1889.
Mwaka 2017 umekuwa wa kutisha na ulioghubikwa na dhuluma kubwa dhidi ya watoto waishio katika maeneo yenye migogoro, huku idadi ya visa vya ukatili na ukiukwaji wa haki zao vikiongezeka kuliko mwaka uliotangulia.
Mtaalamu maalum wa umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Eritrea, ameelezea wasiwasi wake kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo pamoja na mvutano wa mpaka unaondelea kati ya Eritrea na jirani yake Ethiopia.
Wanyama wanahusihwa kwa asilimia 20 kwenye matangazo ya biashara na hata filamu, lakini hawalipwi ujira wowote au kupewa msaada wanaouhitaji, sasa umewadia wakati wa kuwatendea haki.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, leo Alhamisi akiwa mjini Moscow nchini Urusi amesema, kuwa na taasisi imara duniani ni muhimu katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, ugaidi na changamoto nyinginezo.
Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix ametaka ushirikiano zaidi katika kukabiliana na changamoto zinazokabili shughuli za polisi wa chombo hicho, UNPOL, wanaohudumu kwenye operesheni za ulinzi wa amani.
Hatua ya Hungary ya kufanya hali ya kutokuwa na makazi kuwa ni kosa la jinai na ni ya kikatili na isiyoendana na sheria za kimataifa za haki za kibinadamu.
Rais wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Vojislav Šuc, amezungumzia hatua ya Marekani kujitoa kwenye chombo hicho akisema ingawa kila nchi ina haki ya kuamua kuhusu uanachama, bado wakati wa sasa ni wa ushirikiano zaidi wa kimataifa na si vinginevyo.
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, limeanza kuwajengea uwezo wataalamu wa kuandaa mipango ya kukabili maafa nchini Tanzania kama njia mojawapo ya kupunguza maafa.