Masuala ya UM

Mkuu wa UN-HABITAT atunukiwa "Tunzo ya Goteberg"

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT), Anna Tibaijuka, ametangazwa kuwa ni mmoja wa washindi watatu wa Tunzo ya Göteberg, kwa michango yao ya kitaifa na kimataifa, katika maamirisho ya huduma ya maendeleo yanayosarifika.

KM atoa mwito wa kuzikomesha chuki za kwenye uwanda wa intaneti

Ijumanne, kwa siku nzima mfululizo, Idara ya Habari ya UM kwa Umma (DPI) ilifanyisha warsha maalumu kuzingatia taratibu za kusitisha zile kurasa za mitandao ya kompyuta zenye kuchochea chuki.

BU laamrisha vikwazo ziada dhidi ya DPRK

Baraza la Usalama limekutana leo adhuhuri, na kupitisha, kwa kauli moja, azimio 1874 (2009) liliopendekeza kuchukuliwa hatua kali za kuweka vikwazo dhidi ya miradi ya kutengeneza silaha za kinyuklia na makombora katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea/Korea ya Kaskazini (DPRK).

Raisi wa Gabon aombolezwa na KM Ban

KM Ban Ki-moon ametoa taarifa maalumu, kwa kupitia msemaji wake, inayobainisha masikitiko yake makubwa juu ya kifo cha Raisi Omar Bongo Ondimba wa Gabon.

UM imepeleka mkono wa taazia kwa kifo cha raisi wa zamani wa Sudan

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Sudan, Ashraf Qazi, leo amepeleka mkono wa taazia kwa umma wa Sudan pamoja na aila ya aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo, Raisi Jaafer Nimeiri, baada ya magazeti kuripoti rasmi taarifa iliotolewa na Serikali Ijumamosi kuhusu kifo cha Raisi Nimeiry. Marehemu Nimeiry alikuwa na umri wa miaka 79 na aliugua kwa muda mrefu ugonjwa usiotambulika.