Masuala ya UM

KM ametoa mwito wa kukomesha mapigano na ghasia kote Afrika

Akiendelea na ziara yake ya Afrika, KM Ban Ki-moon alikutana Alhamisi na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania mjini Dar es Salaam, kwa mazungumzo juu ya masuala mbali mabli, kuanzia uchaguzi ujao nchini humo, mizozo ya kikanda na janga la uchumi duniani.

KM ameanza ziara ya mataifa matano ya Afrika

KM wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliwasili Afrika Kusini siku ya Jumanne kuanza ziara yake ya nchi tano za Afrika, itakayomfikisha Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Misri.

KM asisitiza ulazima wa kudhibiti pamoja mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Ijumanne adhuhuri KM Ban Ki-moon, alikutana na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu, na aliwaelezea kuhusu safari yake ya karibuni ambapo alitembelea yale maeneo yenye mizozo; na alizungumzia pia juu ya anuwai ya masuala yenye kukabili usalama na amani ya kimataifa.

KM ahimiza uvumilivu baada ya maandamano Bukini kuzusha vifo

Ijumapili KM Ban Ki-moon, kwa kupitia msemaji wake, ametoa taarifa iliosihi makundi yanayohasimiana Bukini, kujitahidi kusuluhisha tofauti zao kwa amani. Alishtumu vikali fujo na vurugu lilioripuka Ijumamosi katika mji mkuu wa Antananarivo, ambapo inakisiwa watu 28 waliuawa na darzeni kadha walijeruhiwa.

KM kufanya ziara ya ghafla Iraq

KM alizuru Baghdad, na kwenye risala yake alipokuwepo huko aliahidi UM utaendelea kuusaidia umma wa Iraq kwa kila njia kurudisha utulivu na kuimarisha maendeleo yao.

KM afanya ziara ya dharura Afghanistan

Ijumatano KM Ban Ki-moon alifanya ziara ya ghafla katika Afghanistan. Alipokuwepo huko, KM aliahidi UM utaendelea kuchangia, kwa kila njia, kwenye zile huduma za maendeleo zinazotakikana, kidharura, kuimarisha usalama na amani ya taifa.