Masuala ya UM

Vikosi vya AMISOM Usomali vyapongezwa na KM kwa ujasiri wao

KM Ban Ki-moon amerudia tena mwito alioutoa hapo kabla, unaoyahimiza Mataifa Wanachama kuharakisha kuchangisha misaada ya fedha, pamoja na ile misaada inayohitajika kushughulikia usafirishaji wa watu na vitu, au lojistiki, ili kuhudumia bora operesheni za vikosi vya Umoja wa Afrika katika Usomali, yaani vikosi vya AMISOM.

KM asihi "vitendo vya mabavu na vurugu" Ghaza visitishwe, haraka.

KM Ban Ki-moon alizungumza na waandishi habari leo adhuhuri ambapo alisihi Israel na ‘Hamas’ kukomesha, haraka, vitendo vyote vya kutumia mabavu katika Tarafa ya Ghaza, na kuchukua hatua zote zinazohitajika kuwaepusha raia na hatari ya kujeruhiwa na mashambulio:~

"2009 unaashiria mizozo ziada", kuonya KM kwenye mkutano na wanahabari kufunga mwaka

Leo asubuhi, KM Ban Ki-moon alifanyisha kikao maalumu cha kufunga mwaka, na waandishi habari wa kimataifa katika Makao Makuu ya UM. Aliashiria kazi za UM katika mwaka 2009 zitafuatana na ugumu utakaovuka matatizo ya mwaka huu:~