Masuala ya UM

UM walaani mauaji ya mhudumia misaada ya kiutu katika CAR

John Holmes, Makamu KM juu ya Masuala ya Kiutu na Mshauri wa Misaada ya Dharura amelaani vikali mauaji ya Elsa Serfass mfanyakazi wa shirika linalotoa huduma bure za afya la Medecins sans Frontiere, mauaji ambayo yalitukia katika eneo la kaskazini-magharibi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Walinzi wa Amani Duniani

Tangu miaka mitano iliopita, UM uliweka kando tarehe 29 Mei kuwa ni siku ya kuadhimishwa rasmi mchango wa wafanyakazi wa kimataifa, waume na wake, wa kutoka kanda mbalimbali za dunia ambao walitumia ujuzi wao, chini ya bendera ya UM, kulinda na kuimarisha amani ya kimataifa, na kuwapunguzia mateso ya hali duni umma wa kimataifa, pamoja na kuendeleza haki za binadamu na kudumisha huduma za maendeleo katika sehemu kadha wa kadha za ulimwengu.

Ripoti ya mfumo wa vikosi vya amani kwa Darfur imekamilishwa

KM Ban Ki-moon amemtumia Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Mei, Balozi Zalmay Khalilzad wa Marekani na vile vile Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika (AU), ripoti yenye kuelezea, kwa ukamilifu, mfumo wa vikosi vya mseto vya AU na UM vinavyotazamiwa kupelekwa kwenye jimbo la Sudan magharibi la Darfur.

KM kuihimiza jumuiya ya kimataifa kuungana kukabili uchafuzi wa hewa ulimwenguni

KM Ban Ki-moon alihutubia kikao maalumu cha Mkutano wa Kamisheni juu ya Maendeleo ya Kudumu (CSD)kilichofanyika Makao Makuu, na kuhudhuriwa na mawaziri wa mazingira pamoja na wajumbe kadha wengineo wa kimataifa.

UM na AU kuteua Mjumbe Maalumu kwa Darfur

KM wa UM Ban Ki-moon na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Alpha Oumar Konare wameteua pamoja Rodolphe Adada wa Jamhuri ya Kongo kuwa Mjumbe Maalumu atakayewakilisha huduma za amani katika jimbo la magharibi la Sudan la Darfur.

KM kulitaka Baraza la Usalama (BU) kuanzisha mazungumzo ya amani kwa Sahara ya Magharibi

Ripoti ya karibuni ya KM juu ya Sahara ya Magharibi imependekeza kwa Baraza la Usalama kuwaita Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi cha Frente Polisario, kushiriki, bila ya shuruti, kwenye mazungumzo ya kuleta suluhu ya kuridhisha, na ya kudumu, itakayoupatia umma wa Sahara ya Magharibi fursa ya kujichagulia serekali halali ya kuwawakilisha kitaifa.

Jumuiya ya kimataifa yasikitika na kulaani mashambulio ya mabomu Algeria na Iraq

Maofisa wa UM wa vyeo vya juu, wakijumuika na KM Ban Ki-moon walishtumu na kulaani vikali mashambulio maututi yaliotukia majuzi kwenye Bunge la Iraq, Baghdad, ambapo Wabunge kadha walifariki na wingi wengineo kujeruhiwa.

Ziara ya faragha ya KM katika Iraq

KM Ban Ki-moon Alkhamisi alifanya ziara ya fargha ya siku moja katika Iraq. Wakati alipokuwa huko alikutana kwa mazungumzo, mjini Baghdad na Waziri Mkuu Nouri Kamal al-Maliki na kuzungumzia juu ya mchango wa UM katika kuusaidia umma wa Iraq kurudisha utulivu wa amani na maendeleo kwenye taifa lao.

Mapendekezo ya KM kurekebisha shughuli za UM yaungwa mkono na Baraza Kuu

Baraza Kuu la UM Alkhamisi limepitisha maazimio mawili muhimu ya kuunga mkono mapendekezo ya KM Ban Ki-moon ya kuleta mageuzi katika kazi za taasisi hii muhimu ya kimataifa. Azimio la kwanza linalenga Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani (DPKO), na limekusudiwa kuboresha kazi za Idara kwa kuipatia uwezo wa kupeleka haraka vikosi vya UM kulinda amani kwenye maeneo yenye machafuko. Vile vile azimio limetaka kubuniwe Kitengo cha Idara juu ya Huduma za Amani Nje ya Makao Makuu.

Ban Ki-Moon ana matumaini amani kurejea tena Uganda kaskazini

KM Ban ameripoti wiki kuwa na mataraji ya kutia moyo kwamba hali ya utulivu na amani itarejea tena katika Uganda ya Kaskazini, kutokana na juhudi za Joaquim Chissano, Mjumbe Maalumu wa KM kwa maeneo yalioathirika na mapigano na waasi wa kundi la LRA.