Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati dunia ikipambana na janga la mlipuko wa COVIDI-19, changamoto kubwa kabisa kuwahi kuikabili dunia tangu vita vya pili vya dunia, kunashuhudiwa pia mlipuko mwingine wa hatari, ambao ni mlipuko wa taarifa potofu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ametoa wito wa kusitisha mapigano haraka kote duniani na nguvu zote kuzielekeza katika adui mkubwa wa sasa ambaye ni virusi vya Corona, COVID-19.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Tijjani Muhammad-Bande ambaye alichaguliwa kuchukua wadhifa huo mnamo mwezi Septemba mwaka jana 2019, hii leo jumatatu, awewasilisha kwa nchi wanachama, vipaumbele vyake vya mwaka 2020.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres leo Jumatatu amesema migogoro ya mataifa inachangia katika nchi nyingi zaidi kuchukua uamuzi ambao matokeo yake hayatabiriki na yanazua hatari kubwa ya matokeo ya mipango mibovu.
Ikiwa leo ni siku ya televisheni duniani, shirika la mawasiliano la Umoja wa Mataifa, ITU limesema chombo hicho cha mawasiliano kitaendelea kuwa na umuhimu mkubwa katika kuongeza uelewa wa masuala ya mambo miongoni mwa binadamu.
Kuelekea maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa mwakani 2020, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo ametangaza kuwa maadhimisho hayo yatajumuisha mjadala jumuishi wa dhima ya jukumu la ushirikiano wa kimataifa katika kujenga mustakabali utakiwao ulimwenguni.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ameziandikia barua nchi wanachama kuhusu ukata mbaya zaidi kuwahi kukabili chombo hicho chenye wanachama 193 kwa karibu muongo mmoja.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema nchi yake inajitahidi katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na imepiga hatua ingawa bado kuna safari ndefu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres leo Septemba 21 ameungana na vijana na kutoka kote ulimwenguni katika kongamano la aina yake la vijana na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.