Masuala ya UM

Vita ya Ukraine na Urusi: India iko upande wa amani na itasalia huko

India imesema itaendelezeka ahadi zake za ushirikiano wa pande nyingi, wenye ushahidi uliothibitishwa,  uamuzi wa kusambaza chanjo kwa mataifa zaidi ya 100 duniani, kutoa misaada ya maafa kwa wale walio katika taabu, kushirikiana na nchi nyingine, kwa kuzingatia ukuaji wenye kujali mazingira, muungano bora wa kidijitali na upatikanaji wa huduma ya afya.

Nchi yoyote inayojielewa ingefanya kama tulichofanya kulinda watu wetu :Urusi

Tulikuwa tunakabiliwa na nchi za magharibi zilishindwa kuafikiana na huku serikali ya Ukriane ikiwa katika vita dhidi ya wananchi wake huko mashariki, Urusi haikuwa na "chaguo" isipokuwa kuanzisha kile ambacho Serikali inataja kama operesheni yake maalum ya kijeshi, Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo.

Ubinadamu uko njiapanda, ni wajibu wetu kuchukua hatua kuunusuru: Ethiopia

Naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Demeke Mekonnen Hassen amesema dunia inakabiliwa na mitihani mingi hivi sasa na imejikuta ipo njia panda kuanzia suala la mabadiliko ya tabianchi, umasikini uliokithiri, migogoro, ugaidi na mivutano ya kimataifa.

Hakuna taifa lililo bora kuliko lingine, mshikamano wa kimataifa ni muhimu:China

Kila mtu katika hii dunia anategemea amani ili kuweza kuishi, kuwa huru, kuwa na maendeleo na kufurahia maendeleo hivyo ni jukumu la kila mtu na kila nchi kuidumisha amesema Wang Yi Waziri wa mambo ya nje wa China akiwasilisha hotuba yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza Kuu hii leo mjini New York Marekani.

Burkina Faso imejiwekea mpango wa kurejesha utulivu – Rais Damiba

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA77 ukiwa umeingia siku ya nne hii leo, Rais Paul Damiba wa Burkina Faso amesema tayari wamejiwekea mpango mkakati wa kurejesha utulivu nchini mwake wakati huu ambapo anaongoza serikali ya mpito kuanzia kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Januari mwaka huu.

Rais wa Sudan asema deni la nje linairudisha nyuma nchi yake kufikia maendeleo

Deni la nje ni kikwazo kikubwa kinachozuia ukuaji wa kiuchumi na kijamii nchini Sudan na pia linazuia kutimiza malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs amesema leo Rais wa serikali ya mpito wa Sudan Abdel-Fattah AlBurhan Abdelrahman Al-Burhan wakati akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu kikao cha 77 jijini New York Marekani.

Juhudi zetu za pamoja za kupambana na mabadiliko ya tabianchi lazima ziendelee - Uganda 

Mabadiliko ya tabia nchi bado ni moja ya changamoto kubwa ya wakati wetu, ndivyo Jessica Alupo, Makamu wa Rais wa Uganda akiwa anahutubia Mjadala Mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA77 Alhamis jioni, jijini New York, Marekani, ndivyo alivyoanza kueleza kuhusu tatizo la mabadiliko ya tabianchi ambalo sasa ni tishio kwa ulimwengu kuliko wakati mwingine wowote.

Amani inaimarika Sudan Kusini lakini bado tuna changamoto: Agany

Amani nchini Sudan Kusini inaendelea kuimarika huku idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani wameanza kurejea katika makazi yao kwenye maeneo ambako utulivu umerejea na serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha mkataba wa amani unadumiswa amesema makamu wa Rais wa Sudan Kusini Hussein Abdelbagi Akol Agany akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza kuu hii leo mjini New York Marekani.

Vita ya Ukraine imetuletea adha dunia nzima: Azali Assoumani

Rais wa kisiwa cha Comoro Azali Assoumani akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu kikao cha 77 amesema jumuiya ya kimataifa hivi sasa inakabiliwa na changamoto lukuki, kuanzia athari za kiafya kama janga la COVID-19 ambalo linaingia mwaka wa tatu ssasa, mabadiliko ya tabianchi hadi vita ya Ukraine ambayo imeleta adha kwa dunia nzima.

Licha ya vikwazo haramu dhidi ya Zimbabwe, tumeweza kudhibiti COVID-19- Rais Mnangagwa

Nchini Zimbabwe licha ya vikwazo haramu vya kimataifa tulivyowekewa, tumeweza kudhibiti janga la COVID-19, amesema Rais wa taifa hilo la kusini mwa Afrika Emmerson Mnangagwa wakati akihutubia Mjadala Mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani Alhamisi ya tarehe 22 Septemba mwaka 2022.