Mjadala Mkuu wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unafunga pazia leo Jumanne ambapo miongoni mwa nchi za Afrika zitakazohutubia ni Tanzania, ambayo imesema ujumbe wake mkuu kwenye jukwaa hilo ni kueleza kuwa bado ina imani kubwa na chombo hicho chenye wanachama 193.