Masuala ya UM

Nina Imani na uwezo walio nao vijana:Guiterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ana imani na uwezo walionao vijana katika kuleta mabadiliko duniani. Flora Nducha na tarifa zaidi

Uhakika wa chakula ni mtihani mkubwa kwa watu wa jamii za asili: FAO

Uhakika wa chakula umeelezwa kuwa ni changamoto kubwa kwa watu wa jamii za asili hususan wanawake ambao ndio walezi wa familia na jamii.  

Siamini nimeingia tena darasani- mtoto mkimbizi

Ujenzi wa mahema matano katika kambi moja ya wakimbizi wa ndani nchini Syria imeleta nuru kwa watoto ambao waliokosa elimu kwa muda mrefu kutokana na mapigano nchini humo.

Kazi ya polisi wanawake, UN ni zaidi ya ulinzi wa amani:Polisi Tanzania

Polisi wanawake kutoka nchini Tanzania wana mchango mkubwa katika operesheni za ulinzi wa aman iza Umoja wa Mataifa na mara nyingi kazi yao ni zaidi ya kuhakikisha usalama wa raia.

Brazil kwanza timizeni haki za binadamu, kubana matumizi kutafuata-UN

Kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka Brazil kutafakari upya mipango yake ya kubana matumizi na kutoa kipaumbele  kwanza kwa haki za binadamu za watu wake ambao wanaathirika na mipango hiyo ya sera za kiuchumi.

Tutafanya kila tuwezalo kulinda watu dhidi ya Ebola Kivu Kaskazini- WHO

Shirika la afya Ulimwenguni WHO, limesema litafanya kila liwezalo kudhibiti kuenea kwa mlipuko wa Ebola ambao umethibitishwa huko jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Zimbabwe chonde chonde zingatieni ahadi ya amani- Guterres

Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa kutokana na matukio ya ghasia yaliyoibuka nchini Zimbambwe baada ya uchaguzi wa rais na kusababisha vifo vya raia.

Ebola yaibuka Kivu Kaskazini, UN yachukua hatua

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, umewasili jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ili kusaka mbinu za kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Kuoanisha SDGs ni muhimu katika kuyafanikisha-WWF

Utashi wa kisiasa ni msingi muhimu kwa nchi katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030 hivyo ni muhimu kwa serikali kuweka mchakato wa kisiasa katika kuwezesha hilo.

 

Wamiliki wa mifugo Malakal wafurahia huduma kutoka kwa walinda amani

Huduma za matibabu kwa wanyama zinazotolewa na walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini, zimeleta nuru kwa wakazi ambao wanategemea mifugo yao kwa ajili ya lishe na kujipatia kipato.