Masuala ya UM

Miradi ya viwanda yatishia uwepo wa watu na wanyama Bangladesh

Bangladesh isitishe mara moja miradi yake ya viwanda kwenye msitu wa akiba wa Sundarbans ambao msitu mkubwa zaidi duniani wenye mikoko, amesema mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu na mazingira, John H. Knox.

Urafiki na mshikamano vyaweza kuinusuru dunia:UN

Dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi, migogoro na shinishizo ambazo zinasababisha mgawanyiko katika jamii umesema leo Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya urafiki.

IOM yatoa dola elfu 75 kusaidia waathirika wa mafuriko Lao

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, limetoa dola elfu 75 kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na kupasuka kwa kingo za bwawa la maji la kuzalisha umeme la  Xenamnoy huko  jimbo la Champassak kusini magharibi mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya  watu wa Lao .

 

WFP na serikali ya Tanzania kushirikiana kuwainua wakulima na wanaohitaji msaada wa chakula

Serikali ya Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula diuniani WFP, wameafikiana kuhusu ubia ambao utawanufaisha wakulima wadogo wadogo wa Tanzania na maelfu ya watu wanaohitaji na kupokea msaada wa chakula  wa WFP barani Afrika.

Nalaani vikali shambulio la kigaidi Sweida, huku ni kupuuza uhai wa watu:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea mjini Sweida Syria siku ya Jumatano.

Maeneo mapya 24 kujiunga na mtandao wa hifadhi ya urithi wa dunia wa UNESCO

Baraza la kimataifa la uratibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kuhusu mpango wa binadamu na mazingira, leo limeongeza maeneo mapya 24 kwenye mtandao wa hifadhi ya urithi wa dunia (MAB) katika mkutano unaoendelea mjini Palembang nchini Indonesia.

Ukatili unaoendelea Cameroon unasikitisha na kuhuzunisha-Zeid

Serikali ya Cameroon imetakiwa  kufanya uchunguzi huru na wa kina dhidi ya ripoti kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na vikosi vya usalama na magenge  yenye silaha dhidi ya maeneo ya wazungumzaji wa kiingereza nchini humo.

Baada ya miaka 6 Tanzania yaaga UNBOA na kukabidhi ujumbe kwa Chile

Tanzania imemaliza muda wake wa miaka sita wa kuwa mjumbe wa Bodi ya ukaguzi wa hesabu ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) na kukabidhi kijiti hicho kwa nchi ya Chile.

Mlipuko wa Ebola kwaheri DRC: Tedros

Shirika la afya ulimwenguni WHO, kwa ushirikiano na wizara ya afya ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo   DRC, leo wametangaza rasmi kumalizika kwa  mlipuko wa Ebola katika jimo la Equateur nchini humo  baada ya jitihada za zaidi ya miezi miwili za kuudhibiti ugonjwa huo.

Zimbabwe ni lazima kuheshimu haki zabinadamu wakati wa uchaguzi:UN

Uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe unakaribia na wito umetolewa leo kwa wadau wote serikali, vyama vya kisiasi na wafuasi wao kuhakikisha kuwauchaguzi huo unafanyika katika mazingira  ya amani, utulivu , kuzingatia haki za binadamu na utawala wa sheria.