Masuala ya UM

Utandawazi umezidisha pengo la usawa duniani-Guterres

Hali ya sasa ya kutokuwa na usawa duniani, kwa njia moja au nyingine, imechochewa na utandawazi.
Ameyasema hayo  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres,wakati akitoa mhadhara kuhusu aliyekuwa Katibu Mkuu wa pili wa umoja huo, DagHammaeskjold, ambaye aliaga dunia mwaka 1961.

 

Dunia tuliyonayo ni moja tu hakuna haja ya kuiharibu-Guterres

Sisi binadamu hatuna rukhsa  ya kuangamiza hii dunia moja tuliyo nayo, ama kukubali tofauti zetu kusababisa mateso na maumivu ambayo yanatuzuia kufaidika na manufaa ya ustaarabu.

Maeneo mapya ya urithi wa kilimo yatajwa na FAO

Maeneo mapya 13 ya urithi wa kilimo yametajwa  na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na kutambuliwa rasmi kama mifumo ya urithi wa kilimo muhimu duniani-GIAHS.

Misukosuko ya ardhi yetu yatukera- Endorois

Jamii ya asili wanahaha kila uchao kuhakikisha kwamba wanapata haki yao ya msingi hususan ile ya ardhi. Jamii hii hukumbwa na misukosuko mingi hasa inapodai haki ya ardhi yao ya asili ambayo ina maana kubwa kwao kuliko inavyofikiriwa.

Viwango vipya vya kudhibiti wadudu wa mimea vyapitishwa: FAO

Mkataba wa kimataifa wa kulinda mimea IPPC leo umeidhinisha viwango vipya venye lengo la kuzuia wadudu waharibifu katika kilimo na mazingira kuvuka mpaka na kusambaa kimataifa.

Hakuna aliyezaliwa gaidi duniani ni mkanganyiko wa mambo:Guterres

Hakuna mtu aliyezaliwa gaidi na hakuna sababu yoyote inayohalalisha ugaidi. Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano wa 16 wa bodi ya ushari ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi unaofanyika Saudia.

Tumechukua hatua kurahisisha maisha ya wakazi wa mijini- Kenya

Mkutano wa 51 wa kamisheni ya idadi ya watu ya Umoja wa Mataifa ukikunja jamvi hii leo jijini New York, Marekani, serikali ya Kenya imejinasibu hatua ambazo imechukua kuhakikisha kuna miji endelevu inayorahisisha maisha ya wakazi wa mijini.

Ajali za barabarani ni janga- UN yaanzisha mfumo maalum

Ajali za barabarani siyo tu zinaleta misiba kwa familia ambazo ndugu au jamaa na marafiki wamepoteza maisha bali pia zinasababisha umaskini kwa sababu fedha zinatumika kwa ajili ya matibabu na wakati mwingine mali hupotea na hivyo mhusika kulazimikakuanza upya maisha.

Watu zaidi ya 250 wapoteza maisha kwenye ajali ya ndege Algeria

Abiria zaidi ya 250 na wahudumu wa ndege wamepoteza maisha leo asubuhi katika ajali mbaya iliyohusisha ndege ya kijeshi nchini Algeria. 

Mali zingatieni ratiba ya uchaguzi

Mkataba wa amani nchini Mali usigeuzwe soka la kisiasa bali utekelezwe ili kufanikisha masuala ya msingi ikiwemo uchaguzi mkuu mwaka huu.