Masuala ya UM

Uzalishaji wa mafuta ya kisukuku unapeleka kombo malengo ya mabadiliko ya tabianchi:UNEP

Licha ya kuongezeka kwa matarajio ya mabadiliko ya tabianchi na ahadi za kutokomeza kabisa uzalishaji wa hewa ukaa, serikali bado zina mpango wa kuzalisha zaidi ya mara mbili ya kiwango cha nishati kutoka kwenye mafuta ya kisukuku ifikapo mwaka 2030, kuliko kiwango ambacho kitapunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia kiwango kilichowekwa kwenye mkataba wa Paris cha nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha Selsiasi (1.5° C)

Uingereza yaahidi dola milioni 4 kwa WFP kusaidia waathirika wa ukame Madagascar

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limeishukuru serikali ya Uingereza kwa mchango wa pauni milioni 3 sawa na dola za Kimarekani milioni 4.1 kwa shirika hili ili liwasaidie kwa chakula watu walioathirika na ukame katika majimbo ya Androy, Anosy na Atsimo Andrefana, Kusini mwa Madagascar.

Afrika inakabiliwa na hatari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi:WMO

Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika mbalimbali na kuratibiwa na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO imesema mabadiliko ya mifumo ya mvua, kuongezeka kwa joto na hali mbaya ya hewa kumechangia kuongezeka kwa ukosefu wa chakula, umaskini na watu kutawanywa barani Afrika mwaka 2020 huku hali mbaya ikizidishwa nachangamoto za kijamii, kiuchumi na kiafya ziliyosababishwa na janga la COVID-19.

Baada ya miaka 10 ya madhila ya vita famililia Syria ziko hoi:Grandi

Kamishna mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Filippo Grandi amerejea kutoka nchini Syria na kutoa ombi jipya la kuongeza misaada ya kibinadamu, wakati mchakato wa rasimu ya katiba mpya ya Syria ukianza wiki hii. 

Taliban yaunga mkono kampeni ya WHO ya chanjo ya polio

Uamuzi wa uongozi wa Taliban wa kuunga mkono kampeni ya nyumba kwa nyumba ya chanjo dhidi ya polio nchini Afghanistan umekaribishwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.

Haki ya mazingira safi na yenye afya: Mambo 6 unayohitaji kufahamu

Tarehe 8 Oktoba, sauti ya makofi makubwa na yasiyo ya kawaida ilisikika karibu na chumba cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi. Vita vilivyopiganwa kwa miongo kadhaa na wanaharakati wa mazingira na watetezi wa haki, mwishowe vilizaa matunda. 

Msimu wa baridi ukijongea hali yazidi kuwa mbaya Afghanistan:UNHCR

Mgogoro wa kibinadamu unazidi kuwa mbaya nchini Afghanistan na ufadhili wa fedha unahitajika haraka ili kusaidia watu milioni 20 limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. 

Nguvu ya mtoto wa kike inasaidia kupunguza pengo la usawa wa kidijitali mtandaoni:UN

Pengo la kijinsia duniani kulingana na utumiaji wa mtandao linaendelea kuongezeka, lakini kuanzia Syria hadi Costa Rica, wasichana wanazidi kupambana kujaribu kupunguza pengo hilo. 

Kenya yachukua Urais wa Baraza, Balozi Omamo atoa msimamo kuhusu wakimbizi

Kenya ambayo imechukua urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Oktoba imesema itakuwa na mikutano minne ya ngazi ya juu ambapo miwili itahutubiwa na Rais Uhuru Kenyatta ilhali mingine miwili itakuwa ni ngazi ya mawaziri na kuhutubiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa taifa hilo la Afrika Mashariki Balozi Raychelle Omamo.
 

UN yashiriki maonesho Dubai Expo 2020:Mambo 5 ya kuyafahamu

Maonesho ya Dubai ya 2020 au Dubai Expo 2020 yaliyocheleweshwa kutokana na janga la COVID-19, ni maonesho ya kwanza kufanyika Mashariki ya Kati, yamefunguliwa rasmi leo Ijumaa 01 Octoba 2021.