Masuala ya UM

KM ahimiza mchango ziada wa mataifa tajiri kuimarisha maendeleo ya nchi maskini

Kwenye mkutano na waandishi habari uliofanyika Davos, Uswiss, KM Ban Ki-moon alitoa mwito maalumu wenye kusihi mataifa matajiri kutowasahau wanadamu wenziwao katika nchi maskini, hasa katika kipindi ambacho maendeleo ya uchumi yamepwelewa na yanaendelea kuporomoka duniani.

Siku ya kumbukumbu dhidi ya maangamizi ya halaiki inahishimiwa kimataifa

Tarehe 27 Januari inaadhimishwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya kumbukumbu za waathirika wa maangamizi makuu ya wanadamu, hususan yale maangamizi ya wafuasi wa Kiyahudi yaliotukia baada ya Vita Kuu ya Pili.

Mukhtasari wa shughuli katika BU

Baraza la Usalama leo asubui linazingatia Operesheni za Kulinda Amani za UM katika Cote d’Ivoire pamoja na Ripoti ya KM juu ya suala hilo.

KM azuru Ghaza na kupendekeza kufanyike uchunguzi juu ya mashambulio dhidi ya UM

KM wa UM Ban Ki-moon, alikutana leo kwenye mji wa Jerusalem, na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na kumwelezea faraja aliyopata baada ya kutangazwa ilani ya upande mmoja ya kusitisha mapigano.

KM akutana na BU kabla ya kuelekea Mashariki ya Kati kusailia Ghaza

Baada ya kuonana na Baraza la Usalama asubuhi ya leo, KM Ban Ki-moon alitarajiwa kuanza ziara maalumu ya Mashariki ya Kati kwa lengo la kuongeza juhudi za kimataifa, katika kutafuta suluhu ya kudumu juu ya mzozo ulioselelea hivi sasa kwenye eneo liliokaliwa, la mapigano, la WaFalastina katika Tarafa ya Ghaza.

Haki za binadamu zakiukwa Ghaza, inasema UM

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu baada ya majadiliano ya siku mbili, kwenye kikao cha dharura, Ijumatatu mjini Geneva limepitisha azimio lenye kulaani vikali operesheni za kijeshi zinazoendelea sasa hivi za vikosi vya Israel kwenye eneo liliokaliwa la WaFalastina la Ghaza.

Suluhu ya mzozo wa Ghaza ipo na UM, asisitiza KM

Imetangazwa asubuhi ya leo kwamba KM Ban Ki-moon atakutana, Ijumanne, na mawaziri wa nchi za kigeni wa kutoka mataifa ya KiArabu, pamoja na wadau wengine muhimu, ili kutathminia taratibu za pamoja za kuhamasisha Baraza la Usalama kuchukua hatua za haraka ili kusitisha mapigano katika Ghaza, na kuiwezesha jumuiya ya kimataifa kuhudumia vizuri zaidi misaada ya kiutu, kwa