Masuala ya UM

KM kulitaka Baraza la Usalama (BU) kuanzisha mazungumzo ya amani kwa Sahara ya Magharibi

Ripoti ya karibuni ya KM juu ya Sahara ya Magharibi imependekeza kwa Baraza la Usalama kuwaita Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi cha Frente Polisario, kushiriki, bila ya shuruti, kwenye mazungumzo ya kuleta suluhu ya kuridhisha, na ya kudumu, itakayoupatia umma wa Sahara ya Magharibi fursa ya kujichagulia serekali halali ya kuwawakilisha kitaifa.

Jumuiya ya kimataifa yasikitika na kulaani mashambulio ya mabomu Algeria na Iraq

Maofisa wa UM wa vyeo vya juu, wakijumuika na KM Ban Ki-moon walishtumu na kulaani vikali mashambulio maututi yaliotukia majuzi kwenye Bunge la Iraq, Baghdad, ambapo Wabunge kadha walifariki na wingi wengineo kujeruhiwa.