Masuala ya UM

UM na Iraq wametiliana sahihi mkataba mpya wa ushirikiano

UM umetiliana sahihi na Serikali ya Iraq mkataba wa ushirikiano wa kihistoria uliofafanua namna UM utakavyohusishwa, katika miaka mitatu ijayo, kwenye juhudi za kufufua shughuli za ujenzi wa Iraq baada ya utulivu kuridishwa kitaifa, na katika kukuza maendeleo na kukidhi mahitaji ya kiutu kwa umma kijumla.

Hapa na Pale

Wajumbe wa kamati mbili za kufuatilia utekelezaji wa Maafikiano ya Djibouti kuhusu Amani Usomali wametangaza kwamba watakutana mwisho wa wiki katika Djibouti, kwa mara nyengine tena, kuzingatia masuala ya kurudisha utulivu na amani nchini.

Wataalamu wa mazao wakutana Vienna kutahminia taratibu mpya za kukithirisha mavuno

Mashirika ya UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) na pia Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) yametayarisha warsha maalumu mjini Vienna, Austria ambao unafanyika kuanzia tarehe 12 Agosti mpaka 15, kuzingatia taratibu mpya za kurekibisha uzalishaji wa mimea, mpango unaotarajiwa kukuza mavuno kwa wingi kusaidia nchi masikini. Kama inavyoeleweka katika miezi ya karibuni makumi milioni ya umma wa kimataifa wanakhofiwa huenda wakazama kwenye janga la njaa na ufukara kwa sababu ya mgogoro wa chakula na nishati ulimwenguni.

KM ahimiza vijana wahusishwe kudhibiti athari za hali ya hewa katika Siku ya Kimataifa kwa Vijana

UM unaadhimisha tarehe 12 Agosti kuwa ni \'Siku ya Kimataifa kwa Vijana\'. Risala ya KM kuiheshimu siku hiyo imetilia mkazo zaidi umuhimu wa kuwahusisha vijana kwenye juhudi za kupiga vita na kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani, madhara ambayo vile vile huzusha matatizo ya njaa.

Hapa na Pale

KM ameripoti kuchukizwa hadi na ripoti aliyopokea kuhusu matokeo ya upelelezi wa Ofisi ya UM Kuchunguza Makosa ya Huduma za Ndani, ambayo ilifichua ushahidi unaojitosheleza kuhusu vitendo vya makansdamizo ya kijinsia yalioendelezwa siku za nyuma na moja ya vikosi vya Bara Hindi vilivyoambatishwa na Majeshi ya Ulinzi wa Amani ya UM katika JKK (MONUC).

Hapa na Pale

Shirika la Mchanganyiko juu ya Ulinzi Amani la UA/UM (UNAMID) limeripoti moja ya helikopta zake ilipigwa risasi adhuhuri katika Darfur Magharibi, nusu saa baada ya kupaa kutokea mji wa El Geneina. Rubani wa helikopta alilazimika kutoendelea na safari na kuamua kurejea El Geneina, kilomita 90 kutoka eneo la tukio hilo. Hakuna mtu aliyejeruhiwa na helikopta inafanyiwa uchunguzi. Haijulikani sasa hivi ni nani aliyehusika na kiutendo hicho.

BU limeshindwa kukubaliana tamko la suluhu juu ya mapigano ya Ossetia Kusini

Baraza la Usalama lilikutana Alkhamisi usiku kwenye kikao kilichoitishwa na Urusi kuzingatia mapigano yaliofumka katika jimbo liliojitenga la Ossetia Kusini katika Georgia, mkutano ambao ulifanyika kuanzia kuanzia saa tano hadi saa nane usiku.

Siku Kuu ya Wenyeji wa Asili kuadhimishwa kimataifa

UM na mashirika yake yamejumuika kuiheshimu \'Siku ya Kimataifa ya Watu wa Asili wa Dunia\' leo Ijumaa. Mada inayotiliwa mkazo katika taadhima za mwaka huu ni ile ya kukuza juhudi za upatanishi baina ya Mataifa wanachama na wenyeji raia wa asili. Taadhima rasmi za \'Siku ya Kimataifa kwa Wenyeji wa Asili\' hufanyika kila mwaka mnamo tarehe 09 Agosti, siku ambayo mwaka huu inaangukia Ijumamosi. ~

Hapa na Pale

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti wiki iliopita lilifanikiwa kuendeleza operseheni ya kuwachanja watoto, karibu milioni mbili, chini ya umri wa miaka mitano, nchini Zimbabwe.

Hapa na Pale

KM ameripoti kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa hali ya vurugu katika jimbo la Ossetia Kusini, Georgia. KM ameyanasihi makundi yote yanayozozana kwenye eneo hilo kujizuia kuchochea vitendo vitakavyopalilia uhasama na kuhatarisha utulivu wa eneo.~~