Masuala ya UM

KM amewasili Philippines kuanza ziara ya mataifa manne Asia

KM Ban Ki-moon Ijumanne amewasili Manila, Philippines, taifa la kwanza miongoni mwa nchi nne za Asia ambazo anatarajiwa kuzizuru rasmi karibuni, ikijumlisha pia Bara Hindi, Nepal na Bangladesh.

Matukio katika Makao Makuu

Baraza Kuu la UM leo limezingatia ripoti ya Shirika la Kimataifa Juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Kinyuklia (IAEA). Kadhalika Baraza linatarajiwa kuchagua wajumbe 20 wa Kamati ya Ushauri wa Miradi ya UM. Mwishowe, Baraza la Usalama limekutana asubuhi kuzingatia hali ya usalama katika Cote d’Ivoire na hali ya wasiwasi iliofumka nchini karibuni wakati taifa hilo linajiandaa kufanyisha uchaguzi. ~

Wajumbe 18 wamechaguliwa na Baraza Kuu kutumikia ECOSOC

Baraza Kuu la UM limeteua wajumbe 18 kutumika kwenye Halmashauri ya Uchumi na Jamiii (ECOSOC), moja ya chombo muhimu cha UM, kwa miaka mitatu ijayo kuanzia Januari 2009.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania atathminia kikao cha 63 cha BK la UM (Sehemu ya II)

Mnamo mwisho wa Septemba, kwenye majadiliano ya wawakilishi wote ya Baraza Kuu la UM, Mwakilishi wa Tanzania, Raisi Jakaya Kikwete, alizungumza kwa niaba ya makundi mawili – taifa lake na pia Umoja wa Afrika – kwa sababu Tanzania hivi sasa vile vile imekabidhiwa madaraka ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.~~

BK limechagua wajumbe wapya kwa Baraza la Usalama

Kikao cha wawakilishi wote katika Baraza Kuu kilichoitishwa kuteuwa nchi tano zisio wanachama wa kudumu kuwakilishwa katika Baraza la Usalama limechagua mataifa ya Austria, Mexico, Ujapani, Uturuki na Uganda kuwa wanachama wapya wa Baraza la Usalama kwa miaka miwili, kuanzia Januari 2009.~ ~

Mukhtasari wa harakati za Baraza Kuu

Mikutano kadhaa ya kamati za Baraza Kuu la UM inaendelea kusailia masuala mbalimbali hapa Makao Makuu kama ilivyoandaliwa ndani ya ajenda ya kikao cha 63 cha mwaka huu cha Baraza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania atathminia kikao cha 63 cha Baraza Kuu la UM

Taarifa ya wiki hii inazingatia tathmini ya Waziri wa Mambo ya ~na Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bernard Membe, juu ya kikao cha 63 cha Baraza Kuu la UM. ~~

Kamati ya Nne imeafikiana kusailia amani, ukoloni na masuala maalumu ya kisiasa

Kamati ya Nne ya Baraza Kuu inayozingatia Masuala Maalumu ya Kisiasa na Kuondosha Ukoloni ilikutana kwenye mkutano mfupi Alkhamisi, na ilipitisha ajenda ya kusailiwa kwenye kikao cha mwaka huu, ambapo zaidi ya mada 12 zitajadiliwa, zikijumuisha vie vile masuala juu ya matumizi ya amani ya sayari nyengine, nje ya dunia, operesheni za ulinzi amani za UM na uondoshaji wa ukoloni kwenye Maeneo Yasiojitawala. ~

D’Escoto apendekeza demokrasia irudishwe tena kwenye UM

Raisi wa kikao cha 63 cha Baraza Kuu la UM, Miguel D’Escoto kwenye mazungumzo na Redio ya UM pamoja na Kituo cha Habari cha UM alihimiza kwa kusema kwamba wakati umewadia kwa Mataifa Wanachama kuhakikisha demokrasia inarudishwa tena katika kuendeleza shughuli za UM.

Jumuiya ya kimataifa inahitajia ushirikiano wa pamoja kulinda watumishi wa UM duniani

Ripoti mpya ya KM iliotolewa Ijumatano kuhusu usalama wa wafanyakazi wake ulimwenguni, imetilia mkazo kwamba kunahitajika “ushirikiano wa karibu sana, wa dharura, na uwajibikaji wa pamoja” kati ya UM na Mataifa Wanachama ili kuhakikisha watumishi wa UM, pamoja na wale wafanyakazi wanaohudumia misaada ya kiutu ulimwenguni, hupatiwa hifadhi kinga na usalama kunusuru maisha.