Masuala ya UM

BU haitoidhinisha utumiaji nguvu dhidi ya shughuli za nyuklia za Iran

Balozi Vitaly Churkin wa Urusi, Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Machi, aliwaambia wanahabari wa kimataifa Ijumanne kwamba vikwazo vilioekewa Iran kwa kutositisha usafishaji wa maadini ya yuraniamu, ambayo hutumiwa kuzalisha nishati ya nyuklia, haimaanishi hata kidogo Baraza hilo litaunga mkono matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya Iran, na kuilazimisha kuyatekeleza mapendekezo ya maazimio yanayohusu tuhuma za kutengeneza silaha za nyuklia.

Maxwell Gaylard ameteuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa UM juu ya Mashariki ya Kati

Maxwell Gaylard, wa Australia ameteuliwa na KM kuwa Naibu Mshauri Maalumu juu ya Masuala ya Mashariki ya Kati, hususan katika usimamizi wa zile shughuli zinazohusu maendeleo na ugawaji wa misaada ya kiutu kwenye maeneo yaliokaliwa kimabavu (OPT) na Israel ya Wafalastina.

BU kuamrisha vikwazo ziada dhidi ya Iran

Baraza la Usalama Ijumatatu alasiri lilikutana kushauriana juu ya suala la udhibiti bora wa silaha za nyuklia duniani. Baada ya mashauriano kumalizika, wajumbe wa Baraza walijadilia mradi wa Iran unaohusu usafishaji wa madini ya yuraniamu halisi, kutumiwa katika uzalishaji wa nishati ya nyuklia. Wajumbe waliafikiana kupitisha azimio jipya, nambari 1803 (2008) ambalo liliamrisha kuanzishwa duru nyengine ya vikwazo dhidi ya Iran, kwa sababu ya Iran kukataa kusitisha mradi wa kuzalisha nishati ya nyuklia kama ilivyoidhinisha Baraza.

Mkuu wa UNHCR azuru kambi za wahamiaji Afrika Mashariki

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), Ijumatatu alianza ziara ya siku nane kutembelea Tanzania na Uganda, ambapo anatazamiwa kufanya mapitio kuhusu namna shughuli zinavyoendelezwa kwenye mataifa haya mawili katika kuwasaidia kihali wahamiaji muhitaji waliopo huko.

KM alisihi Baraza la Haki za Binadamu kuyakamilisha matarajio ya umma

Ijumatatu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alihutubia rasmi mjini Geneva kikao cha cha saba cha Baraza la Haki za Binadamu. Kwenye hotuba yake ya ufunguzi alisema ni wajibu wa Baraza hilo, kuhakikisha kazi zake zinaambatana na matarajio waliyonayo jamii ya kimataifa juu ya taasisi hiyo.

Mjumbe wa KM kuonana na viongozi wa Serikali Usomali

Wiki hii Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah alifanya ziara ya siku tatu kwenye taifa hilo liliopo Pembe ya Afrika. Alipozuru Baidoa, palipo kikao cha Serikali ya Mpito, Ould-Abdallah alichukua fursa ya kuhutubia bunge.

Duru ya nne ya mazungumzo ya Sahara ya Magharibi yakaribia

Duru ya nne ya mazungumzo juu ya kura ya maoni kwa Sahara ya Magharibi yanatazamiwa kufanyika katika mji wa Manhasset, New York kuanzia tarehe 16 hadi 18 Machi.

Raia wa Chad waliokimbilia Cameroon wahamishwa tena kwenye kambi mpya

Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti wahamiaji 5,500 waliokimbia mapigano mwanzo wa mwezi kutoka mji wa N’Djamena, Chad na ambao walikuwa wakiishi kwenye makazi ya muda kaskazini-mashariki ya Cameroon, hivi sasa wamepelekwa uhamishoni kwenye kambi mpya ziliopo kijiji cha Maltam, kitendo ambacho kinatazamiwa kurahisisha ugawaji wa misaada ya kihali kwa umma husika kutoka mashirika ya kimataifa.Kadhalika uhamisho huu utayawezesha mashirika yanayohusika na misaaada ya kiutu kuwapatia wahamiaji hawo hifadhi kinga. Jumla ya wahamiaji 30,000 wa Chad hivi sasa wanaishi kwenye maskani ya muda katika eneo la Cameroon kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Chad asailia hali nchini

Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Ahmad Allam-Mi Ijumanne alasiri alizungumza na waandishi habari waliopo Makao Makuu, baada ya kuhutubia kikao kisichokuwa rasmi cha Baraza la Usalama, kilichojadilia hali, kwa ujumla, nchini kwao.

Eritrea imekakamaa kuiwekea UNMEE vikwazo

Shirika la Ulinzi wa Amani Mipakani Ethiopia/Eritrea (UNMEE) limearifu kwamba wanajeshi wa Eritrea bado wanaendelea kuwaekea vikwazo dhidi ya shughuli zake. UNMEE ilitoa mfano wa kitendo kilichotukia juzi ambapo magari 8 ya UM yalizuiliwa kuelekea mji wa Asmara kukusanya vifaa vya uhamisho wa muda vya watumishi wa UNMEE waliotarajiwa kupelekwa taifa jirani la Ethiopia.