Masuala ya UM

Mtaalamu Huru juu ya Haki za Binadamu katika Usomali alaani vikali mauaji ya kihorera ya raia nchini

Ghanim Alnajjar, Mkariri Mtaalamu Huru juu ya Haki za Binadamu katika Usomali, amenakiliwa akisema mjini Geneva kuwa amechukizwa na kushtushwa sana kwa kuongezeka vurugu na kuharibika kwa haki za kimsingi za raia nchini Usomali, kufuatilia mapigano makali yaliozuka majuzi kati ya vikosi vya Serikali ya Mpito, inayosaidiwa na Jeshi la Ethiopia, dhidi ya vikundi wapinzani wa serikali.

KM kuyazuru mataifa ya Afrika Magharibi kutathminia huduma za amani na MDGs

Baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Shirika la UM juu ya Maendeleo na Biashara (UNCTAD) unaofanyika Accra, Ghana, KM Ban Ki-moon aliendelea na ziara rasmi ya kutembelea mataifa ya Afrika ya Magharibi, ikijumuisha Liberia, Burkina Faso na Cote d\'Ivoire ambako anatarajiwa kutathminia huduma za amani pamoja na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia kwenye maeneo hayo.

Rwanda na JKK zajadiliana namna ya kudhibiti majeshi ya mgambo kwenye maeneo yao

Wawakilishi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, mataifa mawili yaliotia sahihi Taarifa ya Nairobi ya Novemba 2007, walikutana New York Ijumaa iliopita kufanya mapitio kuhusu maendeleo katika juhudi za kudhibiti bora makundi ya waasi na wanamgambo wanaochukua silaha nje ya sheria, yaliokuwepo kwenye maeneo yao.

Tume ya Kudumu ya Wenyeji wa Asili yakutana Makao Makuu katika kikao cha mwaka

Kikao cha Saba cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Masuala ya Haki za Wenyeji wa Asili, kitakachochoendelea kwa wiki mbili, kilifunguliwa rasmi Ijumatatu, Aprili 21 kwenye Makao Makuu mjini New York. Mada ambayo inatarajiwa kupewa umuhimu zaidi mwaka huu ni ile inayoambatana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye tamaduni maumbile na namna inavyodhuru uwezo wa wananchi wa asili kujipatia riziki za kuendesha maisha.

Papa Benedict XVI azuru Makao Makuu ya UM

Papa Benedict XVI leo asubuhi alizuru Makao Makuu ya UM ambapo alikutana na KM Ban Ki-moon pamoja, Raisi wa Baraza Kuu Srgjan Kerim na vile vile wafanyakazi wa UM waliopo mjini New York.

Maharamia Darfur wailazimisha WFP kupunguza posho kwa umma muhitaji

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza leo kwamba kuanzia mwezi ujao wa Mei litalazimika kupunguza kwa nusu, ile posho ya chakula inayopeleka kwenye jimbo la uhasama la Darfur, Sudan kwa sababu malori yalioajiriwa na UM yenye kuchukua shehena ya chakula bado yanaendelea kushambuliwa na maharamia. Vitendo hivi tuliarifiwa huzorotisha sana huduma za kufadhilia misaada ya chakula kwa umma muhitaji katika Darfur.

EthiopiaEritrea: KM anaonya ulinzi wa UM mipakani ukikomeshwa utaruhusu uhasama kurejea

KM wa UM Ban Ki-moon amewasilisha ripoti maalumu majuzi kuhusu operesheni za Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Mipakani Ethiopia/Eritrea (UNMEE), Ripoti imependekeza kwa jumuiya ya kimataifa kuzingatia kidharura changuzi nne muhimu, kusailia kama huduma za amani bado zinahitajika kuendelezwa kwenye eneo la uhasama katika Pembe ya Afrika au zisitishwe, hususan baada ya wenye madaraka Eritrea kuamua kuweka vikwazo kwenye upande wao wa mpaka, hali ambayo ilikwamisha na kozorotisha operesheni za amani za UM.

BU lazingatia uhusiano bora na Umoja wa Afrika

Baraza la Usalama (BU) asubuhi ya leo lilifanyisha kikao maalumu cha hadhi ya juu, kuzingatia taratibu mbadala, zitakazotumiwa kuimarisha uhusiano bora kati ya UM na Umoja wa Afrika, hususan katika huduma za kusawazisha usalama na amani wa kieneo na kimataifa.

Ajali ya ndege katika JKK yaihuzunisha UM

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limethibitisha kwamba ndege ya abiria ya kampuni ya ndege inayoitwa Hewa Bora ilianguka na kupasuka hapo Ijumanne, muda tu baada ya kuanza kuruka, katika mji wa kaskazini-mashariki wa Goma katika JKK. Iliripotiwa na Msemaji wa KM kwamba ndege ilikuwa imebeba abiria na wafanyakazi wa ndege 70 ziada.

Wataalamu wasisitiza kilimo cha kisasa chawajibika kuzingatia mahitaji halisi ya umma masikini

Tume ya Kimataifa Maalumu ya Wataalamu 400 waliodhaminiwa bia na Benki Kuu ya Dunia pamoja na mashirika kadha ya UM, imetoa mwito wa dharura uliojumuishwa kwenye ripoti iliopendekeza kufanyike mageuzi makali ya kimsingi, haraka iwezekanavyo, kwenye taratibu zinazotumiwa kuzalisha mazao ya chakula, ili kuhakikisha marekibisho haya mapya yatakidhi zaidi mahitaji ya watu masikini na wale wenye njaa.