Masuala ya UM

Mukhtasari wa mikutano katika Makao Makuu

Kwenye ukumbi wa Baraza la UM juu ya Uchumi na Jamii (ECOSOC), hii leo, panafanyika majadaliano ya kuzingatia mfumo unaofaa kudhibiti bora mizozo na kuimarisha operesheni za ulinzi amani kimataifa. Kikao hiki kimeandaliwa na Ofisi ya Raisi wa Baraza Kuu la UM pamoja Jumuiya ya Wabunge wa Kimataifa (IPU).

Charlize Theron aidhinishwa rasmi kuwa Mjumbe wa Amani dhidi ya Unyanyasaji wa Wanawake

Mwigizaji wa kike wa michezo ya sinema kutoka Afrika Kusini na Marekani, Charlize Theron leo ameidhinishwa rasmi na kukabidhiwa wadhifa wa Mjumbe Maalumu wa UM kwa Amani, na anatumainiwa kuchangisha huduma zake kwenye juhudi za kukomesha udhalilishaji na utumiaji mabavu dhidi ya wanawake, hususan katika bara la Afrika.~

Kwenye kikao cha kila mwezi na waandishi habari KM azingatia mizozo ya kimataifa, ikijumlisha vurugu la JKK

Leo Ijumanne, KM Ban Ki-moon leo alikuwa na mahiojiano ya kila mwezi na waandishi habari wa kiamataifa waliopo hapa Makao Makuu. Kwenye mkusanyiko huo KM alisailia juhudi za karibuni za kukabiliana na mgogoro wa fedha katika soko la kimataifa, pamoja na kuzingatia matatizo ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Uteuzi wa Barack Obama kuwa raisi mpya Marekani wapongezwa na KM

KM Ban Ki-moon alipokutana na waandishi habari kwenye Makao Makuu ya UM alimpongeza Seneta Barack Obama kwa kushinda uchaguzi wa uraisi katika Marekani:~~

KM asailia uchaguzi Marekani

Hii leo, tarehe 04 Novemba (‘08) makumi milioni ya raia wa Marekani wanashiriki kwenye kura ya kuteua raisi mpya.