Masuala ya UM

Mjumbe wa KM kuonana na viongozi wa Serikali Usomali

Wiki hii Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah alifanya ziara ya siku tatu kwenye taifa hilo liliopo Pembe ya Afrika. Alipozuru Baidoa, palipo kikao cha Serikali ya Mpito, Ould-Abdallah alichukua fursa ya kuhutubia bunge.

Duru ya nne ya mazungumzo ya Sahara ya Magharibi yakaribia

Duru ya nne ya mazungumzo juu ya kura ya maoni kwa Sahara ya Magharibi yanatazamiwa kufanyika katika mji wa Manhasset, New York kuanzia tarehe 16 hadi 18 Machi.

Raia wa Chad waliokimbilia Cameroon wahamishwa tena kwenye kambi mpya

Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti wahamiaji 5,500 waliokimbia mapigano mwanzo wa mwezi kutoka mji wa N’Djamena, Chad na ambao walikuwa wakiishi kwenye makazi ya muda kaskazini-mashariki ya Cameroon, hivi sasa wamepelekwa uhamishoni kwenye kambi mpya ziliopo kijiji cha Maltam, kitendo ambacho kinatazamiwa kurahisisha ugawaji wa misaada ya kihali kwa umma husika kutoka mashirika ya kimataifa.Kadhalika uhamisho huu utayawezesha mashirika yanayohusika na misaaada ya kiutu kuwapatia wahamiaji hawo hifadhi kinga. Jumla ya wahamiaji 30,000 wa Chad hivi sasa wanaishi kwenye maskani ya muda katika eneo la Cameroon kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Chad asailia hali nchini

Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Ahmad Allam-Mi Ijumanne alasiri alizungumza na waandishi habari waliopo Makao Makuu, baada ya kuhutubia kikao kisichokuwa rasmi cha Baraza la Usalama, kilichojadilia hali, kwa ujumla, nchini kwao.

Eritrea imekakamaa kuiwekea UNMEE vikwazo

Shirika la Ulinzi wa Amani Mipakani Ethiopia/Eritrea (UNMEE) limearifu kwamba wanajeshi wa Eritrea bado wanaendelea kuwaekea vikwazo dhidi ya shughuli zake. UNMEE ilitoa mfano wa kitendo kilichotukia juzi ambapo magari 8 ya UM yalizuiliwa kuelekea mji wa Asmara kukusanya vifaa vya uhamisho wa muda vya watumishi wa UNMEE waliotarajiwa kupelekwa taifa jirani la Ethiopia.

Hapa na pale

Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Masuala ya Mgogoro na waasi wa LRA Uganda Kaskazini, Joaquin Chissano, Raisi wa zamani wa Msumbiji, amenakiliwa kuripoti kupatikana maafikiano ya kutia moyo mwisho wa wiki, baada ya Serikali ya Uganda na waasi wa LRA walipotiliana sahihi kwenye mji wa Juba, Sudan Kusini, mwafaka wa kudumisha kuacha kupigana.~

Hapa na pale

Edward Luck, raia wa Marekani ameteuliwa kuwa Mshauri Maalumu wa KM wa UM juu ya masuala yanayohusu hifadhi-kinga na misaada ya kiutu ya dharura penye uhasama wa kitaifa.

Mkutano wa kudhibiti athari za mabadiliko ya hali ya hewa kufunguliwa Monaco

Kikao maalumu cha Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) kinafanyika sasa hivi Monaco kuzingatia sera mpya za kudhibiti bora mazingira kutokana na uharibifu unaochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Mawaziri wa mazingira kutoka Mataifa Wanachama 100 ziada wanahudhuria mkutano.

Baraza la Usalama kujadili hali katika Usomali

Ijumatano Baraza la Usalama litazingatia hali katika Usomali na huenda likapitisha azimio juu ya vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Afrika (UA).

Eritrea imezuia Walinzi wa usalama wa UM kuingia Ethiopia

Wenye madaraka Eritrea wamekataa kuwaruhusu watumishi wa Shirika la UM la Ulinzi wa Amani Mipakani Ethiopia/Eritrea (UNMEE) kwenda Ethiopia, hali ambayo iliwalazimisha kurejea mjini Asmara kusubiri ushauri kutoka UM juu ya hatua za kuchukuliwa nawo baada ya mvutano huu. Tukio la kuwazuia walinzi wa amani kutovuka mpaka limejiri licha ya kuwa Ijumaa iliopita Baraza la Usalama lilishtumu vikali "ukosefu wa ushirikiano" kutoka Serikali ya Eritrea, ambaye ililaumiwa kujitenga na majukumu yake ya kusaidia vikosi vya UNMEE kudhibiti bora usalama kwenye eneo la mgogoro mipakani.