Masuala ya UM

UM kusaidia polisi wa Liberia kufikia viwango vya kimataifa vya haki za binadam.

Mjumbe maalum wa UM huko Liberia amekabidhi kwa Kikosi cha Polisi cha Taifa, jengo lililo karabatiwa upya la kuwaweka wafungu kulingana na masharti muhimu kabisa ya viwango vya kimataifa vya haki za binadam.

Umuhimu wa Umoja wa Mataifa duniani

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw Ban Ki-moon, amesema UM unaigia katika enzi ambayo inaweza kunawiri kwa sababu changa moto kuu duniani zimekua na utata sana, kiwango ambacho mataifa binafsi yanashindwa kuyatanzuwa wenyewe.

Naibu katibu Mkuu atoa mwito wa kusaidiwa mataifa ya Afrika magharibi yaliyokumbwa na vita

Naibu katibu mkuu Asha-Rose Migiro ametowa mwito wa kuungwa mkono zaidi Guinea-Bissau na mataifa mengine katika kanda hiyo, ambayo yana jikokota kutoka hali ya vita. Alisema hayo baada ya kurudi New York, kufuatia ziara yake ya Afrika wiki iliyopita.

Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Afrika

Mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Afrika AU, ulifanyika Accra, Ghana mapema mwezi wa Julai, suala kuu lilikua juu ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa ya Afrika chini ya serekali moja kuu. Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Asha-Rose Migiro aliwahutubia viongozi na kusema kuna changamoto chungu nzima kufikia lengo hilo. ~

Ushirikiano wa Jumuia ya Afrika na Umoja wa Mataifa wasifiwa na Naibu katibu mkuu

Naibu katibu mkuu wa UM, Bi Asha-Rose Migiro yuko ziarani baraani afrika na miongoni mwa mambo muhimu wakati wa ziara yake alihutubia ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa Jumuia ya afrika AU huko Accra Ghana, pamoja na kufungua mkutano wa kimataifa juu ya wanawake huko Nairobi nchini Kenya.

Bi Migiro apongeza ushirikiano wa AU na UM

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa bi Asha-Rose Migiro, amesifu mafanikio katika ushirikiano mzuri kati ya Jumuia ya Afrika AU na UM katika kupatikana usalama na amani na kuendeleza maendeleo.