Kila mara tumekuwa tukimulika shughuli za jumla za walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu katika maeneo mbali mbali duniani iwe ni ujenzi wa barabara, ulinzi wa amani na hata kilimo lakini leo tunaangazia je mlinda amani mmoja mmoja siku yake inakuwa vipi? Na leo tunammulika Luteni Kanali John Ndunguru, Kamanda wa kikundi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT 7, kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO. Anayetuletea ripoti hiyo ni Issa Mwakalambo, Afisa Habari wa TANZBATT 7.