Masuala ya UM

Burkina Faso imejiwekea mpango wa kurejesha utulivu – Rais Damiba

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA77 ukiwa umeingia siku ya nne hii leo, Rais Paul Damiba wa Burkina Faso amesema tayari wamejiwekea mpango mkakati wa kurejesha utulivu nchini mwake wakati huu ambapo anaongoza serikali ya mpito kuanzia kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Januari mwaka huu.

Asante Tanzania mwanangu sasa atajulikana alipozaliwa :Mkimbizi Evangeline

Familia za wakimbizi wa Burundi wanaoishi kwenye kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma nchini Tanzania wameishuru serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki kwa kuwapatia nyaraka muhimu za watoto wao, vyeti vya kuzaliwa wakati wa ziara ya Kamisha Mkuu wa wakimbizi Filippo Grandi iliyokamilika mwishoni mwa wiki.

Vizazi vyote tuungane kuwasaidia vijana : Guterres

Ikiwa leo ni siku ya vijana duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa jamii kuwasaidia vijana kwa kuwekeza kwenye kuwapatia elimu na kuwajengea uwezo wa kiujuzi kupitia mikutano pamoja na kufanya mabadiliko katika mifumo ya elimu.

Cryptocurrency: UNCTAD yatangaza sera 3 zakufuatwa katika matumizi ya sarafu za kidijitali

Kamati ya  Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo UNCTAD imetoa mapendekezo ya sera tatu zinazoweza kutumiwa na nchi zinazoendelea kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya sarafu za kidijitali au Cryptocurrency wakati huu ambapo nchi nyingi hazina sera wala mifumo madhubuti ya udhibiti na matumizi yake kwa jamii.

Meli ya kwanza kutoka Ukraine yakamilisha ukaguzi na kuruhusiwa kuendelea na safari

Meli ya kwanza ya Ukraine iliyobeba shehena ya tani 26,000 za mahindi kwenda kuuzwa nchini Lebanon imekamilisha ukaguzi wake nchini Uturuki na kuruhusiwa kuendelea na safari yake hii leo. 

Walinda amani wa MONUSCO waliouawa katika maandamano DRC waagwa 

Viongozi wa Umoja wa mataifa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kidemoktrais ya Congo, DRC wametoa heshima zao za mwisho kwa walinda amani watano wa kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO waliokufa wakati wa maandamano na uvamizi wa vituo vya ujumbe huo huko Goma na Butembo jimboni Kivu Kaskazini. Walinda amani hao wanatoka Morocco na India ambapo Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Bintou Keita amesema MONUSCO iko tayari kwa mazungumzo ya amani ili kuendeleza na kudumisha amani nchini humo.

Nelson Mandela alikuwa mponyaji wa jamii:Guterres

Wakati dunia hii leo ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini ameonyesha kila mtu kila mahali anao uwezo na wajibu wa kujenga maisha bora ya baadae ya wote. 

Shughuli za uvuvi na ufugaji wa Samaki zinatoa mchango mkubwa kwenye uhakika wa upatikanaji wa chakula :FAO

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari ukiwa katika siku ya tatu hii leo huko Lisbon nchini Ureno Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ongezeko kubwa la ufugaji wa samaki sambamba na uvuvi wa kimataifa umesababisha mazao ya vyakula vya majini kuwa kwenye rekodi ya juu katika kuchangia kwa kiasi uhakika wa chakula na lishe katika karne hii ya Ishirini na moja.

Umoja wa Mataifa utaendelea kusimama na Afrika  

Afrika ni nyumba ya matumaini. Katika Siku ya Afrika, tunasherehekea ahadi kubwa na uwezo wa bara hili lenye utofauti na nguvu. Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya Afrika ambayo huadhimishwa kila tarehe 25 Mei.

Joto laendelea kuongezeka duniani kwa mwaka wa 7 mfululizo: WMO

Viashiria vinne vinavyotumika kupima hali ya hewa duniani vyote vimeonesha hali kuendelea kuwa mbaya duniani licha ya wadau kila uchao kujadiliana na kuahidi kuchukua hatua madhubuti za kulinda dunia kutoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na shughuli za kibinadamu.