Wahisani waliokusanyika mjini Geneva Uswisi hii leo wameahidi dola bilioni 2.6 ili kuhakikisha kwamba operesheni za misaada ya kibinadamu zinaendelea nchini Yemen katika wakati huu ambao msaada ndio tumaini pekee la mamilioni ya Wayemen.
Wakati mkutano kuhusu mzozo wa Yemen unaendelea mjini Geneva Uswisi hii leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limetoa wito kwa wadau wote kutoa kipaumbele kwa suala la ulinzi wa watoto na kuheshimu haki zao za msingi.
Baraza la haki za binadamu limeanza kikao chake cha 40 hii leo mjini Geneva Uswis kikijadili juhudi za kitaifa na kimataifa katika kuchagiza na kulinda haki za binadamu.
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesihi pande kinzani kwenye mzozo nchini Syria ziheshimu sheria za kimataifa pindi zinapoendesha operesheni zao za kijeshi wakati huu ambapo usalama wa raia huko Idlib unazidi kuzorota.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema mwaka jana 2018 mahitaji ya kuwapatia wakimbizi nchi ya tatu ya hifadhi yalikuwa ni chini ya asilimia 5 licha ya kwamba mwaka huo ulivunja rekodi ya idadi ya kubwa ya wakimbizi waliosaka hifadhi ya nchi ya tatu.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya serikali na pande kinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR unaleta matumaini kwa mamilioni ya watoto kwenye taifa hilo lililokuwa limegubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Watu zaidi ya 7,500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) wamekimbilia Uganda kusaka hifadhi kufuatia mashambulizi mapya katika jimbo la Ituri mahsariki mwa nchi hiyo.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inaonyesha ongezeko la ukatili wa kingono katika jimbo la Unity kaskazini mwa Sudan Kusini, ikisema wanawake 134 na wasichana wamebakwa na wengine 41 wamekumbwa na aina nyingine za ukatili wa kingono kati ya Septemba na Disemba 2018.
Takwimu za Shirika la afya ulimwenguni, WHO zinaonyesha kuwa idadi ya maambukizi ya surua inaongezeka katika maeneo mabli mbali na sio changamoto ya bara moja
Mtaalam maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu uhuru wa mahakama na mawakili, Diego Garcia-Sayán, leo ameonya kwamba hatua ya Rais wa Nigeria kumsitisha kazi na kumbadilisha mwanasheria mkuu wan chi hiyo ni kinyume na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu kuhusu uhuru wa mahakama na kutenganisha madaraka.