Ripoti mpya ya pamoja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lila la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula WFP inasema kuwa idadi ya watu walio na njaa duniani imepanda kwa kiasi cha watu millioni 38 kati ya mwaka wa 2015 na 2016. Selina Jerobon na ripoti kamili.
Ripoti mpya iliyotolewa leo imeonyesha kuwa bado kuna shida kubwa katika matumizi sahihi ya mikataba ya biashara huria ambayo Muungano wa Ulaya imetia saini na nchi zingine.
Mkutano wa kawaida wa 30 wa viongozi wa Afrika ukiendelea huko Addis Ababa, Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja mambo matano ya kuimarisha ushirikiano kati a pande mbili hizo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio lililofanyika leo kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul ambako washambuliaji walitumia gari linalofanana na gari la wagonjwa kutekeleza shambulio hilo.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya halaiki dhidi ya wayahudi, Umoja wa Mataifa umesema silaha pekee dhidi ya vitendo kama hivyo ni elimu na uelewa kuhusu maadili ya kibinadamu.