Muungano wa tume ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika umewasili nchini Niger kwa ajili ya kuhakiki hatua zilizopigwa na serikali ya mpito ambayo ilitwaa madaraka mwaka uliopita baada ya kufanya mapinduzi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali tukio la shambulizi la bomu lililowauwawa watu 21 na kuwajeruhi wengine 70 wakati wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa mwaka mpya kwenye kanisa Qiddissin Coptic mjini Alexandria, Misri.