Masuala ya UM

Furaha ndani ya familia iliwafanya kukaribia kuuawa na genge la wahalifu nchini Honduras

Makundi ya wahalifu nchini Honduras yalibadili kabisa maisha ya familia ya Daina na kusababisha kuikimbia nchi hiyo kwenda kuomba hifadhi nchini Mexico. 

Mwaka 2022 tuazimie kujikwamua kutoka majaribuni- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma salamu za mwaka mpya wa 2022 akitaka dunia iazimie kwa pamoja mwaka huu mpya uwe wa kuondokana na majaribu yanayotarajia kuikumba.

FAO yatazamia kufanikisha zaidi Bora 4 mwaka 2022

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO Qu Dongyu ametoa ujumbe wake kwa mwaka mpya wa 2022 huku akitaja mafanikio ambayo shirika hilo limefanikisha mwaka huu wa 2021 licha ya changamoto ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
 

Ushirikiano wa kijeshi kati ya DRC na Tanzania unasaidia sana kuleta amani Beni

Ushirikiano kati ya vyombo vya usalama ikiwemo polisi na FRDC ambalo ni Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu chini ya Mwavuli wa MONUSCO, umeendelea kuzaa matunda kwa kuwahakikishia usalama wananchi wa maeneo ya mashariki mwa DRC. 

Nyumbani ni nyumbani ndio maana tumeamua kurejea:Wakimbizi wa DRC nchini Uganda

Wakimbizi 11,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC waliokimbilia nchi jirani ya Uganda hivi karibuni kufuatia machafuko yanayoendelea Mashariki mwa DRC wameanza kurejea nyumbani kwa hiyari na kilichowasukuma ni usemi wa wahenga kuwa nyumbani ni nyumbani.

COVID-19 ni tishio kubwa kwa maendeleo ya watoto katika historia ya miaka 75 ya UNICEF

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imesema janga la COVID-19 limeleta hali mbaya zaidi kwa watoto kuwahi kushuhudiwa katika historia yake ya miaka 75 nakuzitaka nchi kuongeza juhudi kuwanusuru watoto.

Washindi wa tuzo ya mazingira ya UNEP mwaka 2021 watangazwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani UNEP leo limewatangaza washindi wanne wa tuzo yake ya juu kabisa ya mazingira ijulikanayo kama “champions of the Earth Award” kwa mwaka 2021.

UNHCR yawapa msaada wakimbizi na wahamiaji wa jamii za asili za Warao Guyana

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa wasiwasi mkubwa na mazingira dunia wanaoishi wakimbizi na wahamiaji kutoka jamii ya Warao nchini Venezuela ambao kwa sasa wanaishi Guyana.

Tuna haki ya kushiriki mazungumzo kuhusu tabianchi- Kestia

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linatumia mabalozi wake watoto ambao ni wachechemuzi kuhusu tabianchi kuelezea adha ambazo watoto wanapata kutokana na madhara ya tabianchi na nini wanataka kifanyike. 

Siku ya Kiswahili duniani kuadhimishwa tarehe 7 Julai kila mwaka- UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO leo limeitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.