Kundi la kigaidi la Al Shabbab linaendelea kuwa tishio nchini Somalia wakati serikali ikijaribu kujenga upya taasisi za usalama na kuifanya nchi hiyo kuweza kujitegemea. Hayo yamesemwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating, alipozungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, ingawa pia amesema jitihada mbalimbali za kujenga serikali inayowajibika, na itakayowezesha watu wote zinaendelea.