Janga la corona au COVID-19 linabadili hatua zilizopigwa katika maendeleo na kuujaribu msingi wa amani ya kimataifa, lakini pia linatoa fiursa ya kushirikiana kuzisaidia serikali na jamii kujijenga vyema upya umesema mkutano wa kimataifa ulioanza leo kwa njia ya mtandao mjini Roma Italia ukiwaleta pamoja wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, taasisi za fedha za kimataifa, Muungano wa Afrika naserikali za Muungano wa Ulaya.