Masuala ya UM

ILO Afrika Mashariki yaungana na wenyeji kusherehekea siku ya wafanyakazi

Leo ni siku ya wafanyakazi duniani, au Mei mosi ambapo mataifa ikiwemo yale ya barani Afrika yameadhimisha siku hiyo huku shirika la kazi ulimwenguni ukanda wa Afrika Mashariki likitoa wito kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya kuchagiza usawa, haki kwa jamii na kuimarisha mazingira ya kazi kwa wote. 

Kama maisha hayakupi maana, ala za jazz zitafanya kazi hiyo-Azoulay

Muziki wa Jazz unaelezea maisha na una jukumu muhimu la kuchagiza amani, majadiliano na kuyafanya maisha yawe na maana muhimu kwa watu wote duniani, amesema mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sanyansi na utamaduni UNESCO katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya muziki wa Jazz hii leo.

Teknolojia za watu wa asili kumulikwa wakati wa jukwaa lao New York

Mkutano wa jukwaa la kudumu kuhusu masuala ya watu wa asili unaanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ukileta pamoja zaidi ya watu 1,000 wa  jamii ya watu asili kutoka kona mbalimbali duniani.

Ardhi ya kuazima yamwezesha mkimbizi kutoka Sudan Kusini kulea watoto yatima

Ukarimu wa Uganda wa kuwapatia maeneo ya kilimo wakimbizi kutoka Sudan Kusini, umewezesha wakimbizi kusaidia jamii zinazowazunguka wakiwemo watoto yatima nchini humo.

WFP yahitaji fedha zaidi kufanikisha operesheni zake Msumbiji

Mwezi mmoja tangu kimbunga Idai kipige Msumbiji na kusababisha maafa, shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema limeweza kufikisha msaada wa chakula kwa watu milioni mmoja huku likiendelea kupanua wigo wa msaada na kuwapatiwa wananchi misaada ya kujikwamua. 

UNICEF na TEF wawapa tuzo waandishi 10 kwa uandishi bora wa habari za watoto nchini Tanzania

Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na Jukwaa la wahariri, TEF, wamewatunukia tuzo waandishi wa habari 10 ambao wameangazia kwa ubora habari zinazowahusu watoto katika mwaka 2018/19.

Licha ya mapigano Libya, WHO yaendelea kupeleka vifaa vya matibabu

Wakati mapigano yakishamiri kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli na viunga vyake, huku idadi ya manusura ikiongezeka hadi mamia, shirika la afya ulimwenguni, WHO limechukua  hatua ya haraka kupeleka vifaa vya matibabu vinavyohitajika zaidi.

Wakielimishwa na kujumuishwa Vijana ni chachu kubwa katika SDGs:YUNA

Vijana wanaweza kuwa chachu kubwa katika utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s  mwaka 2030 endapo wataelimishwa kujumuishwa na kupewa fursa. 

Kupambana na aina zote za utapiamlo na kukuza ubunifu katika kilimo ndivyo vipaumbele vya juu vya FAO kwa miaka miwili ijayo.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO José Graziano da Silva katika hotuba yake ya ufunguzi mkutano wa baraza tendaji la shirika huo ulioanza hii leo mjini Roma Italia, amesisitiza kuwa kwa miaka miwili ijayo FAO itajikita katika kukuza mifumo ya chakula cha lishe na uvumbuzi katika kilimo.

Watoto milioni 1.1 Venezuela watahitaji msaada mwaka 2019

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF leo limesema kufuatia mzozo wa Venezuela takriban watoto milioni 1.1 ikiwemo waliolazimika kukimbia kutoka Venezuela, wale ambao wanarejea nyumbani na wale walooko katika jamii zinazowahifadhi au safarini watahitaji ulinzi na huduma za msingi katika ukanda wa Amerika ya Kusini na Carribea mwaka huu wa 2019.