Masuala ya wapiganaji mamluki, ushawishi wa vijana kutumbukia kwenye vitendo vya kigaidi na kitendo cha vijana hao kuona wameenguliwa kwenye masuala yanayowahusu yameangaziwa katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kukabiliana na uagidi ulioanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
Utesaji unasalia kuwa ni kitendo kisichokubalika na kutohalalishwa wakati wowote ule na kwa sababu yoyote ikiwemo wakati wa hali ya dharura, vurugu za kisiasa au hata wakati wa vita
Wanyama wanahusihwa kwa asilimia 20 kwenye matangazo ya biashara na hata filamu, lakini hawalipwi ujira wowote au kupewa msaada wanaouhitaji, sasa umewadia wakati wa kuwatendea haki.
Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix ametaka ushirikiano zaidi katika kukabiliana na changamoto zinazokabili shughuli za polisi wa chombo hicho, UNPOL, wanaohudumu kwenye operesheni za ulinzi wa amani.
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, limeanza kuwajengea uwezo wataalamu wa kuandaa mipango ya kukabili maafa nchini Tanzania kama njia mojawapo ya kupunguza maafa.
Ukatili wa kingono katika migogoro ya vita ni tatizo lililomea mizizi na sio kwa wanawake peke yao, wanaume na watoto wametumbukizwa pia katika zahma hiyo kama anavyofafanua wakili Ann N. Kamunya raia wa Kenya ambaye sasa huyo Ankara Uturuki akifanya kazi na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amehutubia kikao cha 38 cha Baraza la haki za binadamu huko Geneva, Uswisi na kusema kuwa hali ya haki hizo duniani kote sasa si shwar.
Licha ya ugumu ya maisha mkulima mmoja nchini Bangladesh, bado amekuwa na moyo wa kutoa eneo lake la shamba ili kuhifadhi zaidi ya familia 71 za wakimbizi 300 wa Rohingya waliokimbilia nchini humo kutoka Myanmar.