Masuala ya UM

Waliopoteza maisha kutokana na mafuriko Kenya wafika 132: OCHA

Idadi ya waliokufa kutokana na athari za mafuriko nchini Kenya  imepanda. Ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA linasema kuwa hadi sasa idadi ya waliofariki imefikia watu132 huku   zaidi ya 311,000 wameachwa bila makazi.

Bado idadi kubwa ya watoto hawajawahi kunyonya maziwa ya mama: UNICEF

Idadi ya watoto wanaokosa kunyonya maziwa ya mama bado ni kubwa hususan miongoni mwa nchi tajiri duniani umesema uchambuzi mpya uliotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. 

Iran inatekeleza ahadi zinazohusiana na nyuklia:IAEA

Hadi kufikia sasa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA linaweza kuthibitisha kuwa ahadi zinazohusiana na nyuklia zinatekelezwa na Iran.

UN yasikitika Marekani kujitoa makubaliano kuhusu Iran

Guterres ataka shaka na shuku kwenye JCPOA iondolewe kwa kuzingatia mfumo uliowekwa na si kwa pande husika kujitoa kwenye makubaliano hayo yanayolenga kuwezesha Iran kuachana na nyuklia.