Masuala ya UM

Ingawa hatua zimepigwa Afrika kukabili COVID-19, lakini bado kuna changamoto:UNITAID

Bara la afrika limepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya janga la COVID-19, idadi ya wagonjwa na vifo inapungua lakini bado kuna changamoto kubwa kuhusu janga hilo limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu UNITAID ambalo linajikita katika kutafuta suluhu za kibunifu za kuzuia, kutambua na kutibu magonjwa kwa haraka zaidi katika nchi za kipato cha kati na cha chini.

Programu ya UNICEF Uganda yamuepusha mtoto ‘Sarah’ kujiua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Uganda linaendesha programu ya waelimishaji rika ambayo imesaidia watoto kadhaa wa kike akiwemo Sara kuacha kujiua baada ya kubakwa na kupewa ujauzito na hatimaye kurejea shuleni kusoma huku akilea mtoto wake na kuwa na matarajio makubwa kwa siku za usoni

Sakata la UNOPS, Mkuu wake ajiuzulu, Katibu Mkuu aridhia

Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usimamizi wa miradi, UNOPS Grete Faremo amejiuzulu nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kukamilika kwa uchunguzi uliofanywa kubaini madai ya ubadhirifu kwenye ofisi hiyo.

Ziara ya Katibu Mkuu wa UN kuhusu Ukraine: “Nafurahia kuripoti mafanikio fulani“

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonip Guterres amelihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo jioni (05-05-2022) na kueleza kuwa wakati wa ziara yake maalum nchini Urusi na Ukriane hakusita kuwaeleza kinaga ubaga bila kupepesa maneno kwa nyakati tofauti na marais wa nchi hizo kwakuwa anataka kuona mzozo na ukatili unaoendelea sasa unamalizika mara moja. 

Ajenda Mpya ya Miji ni jawabu la Ajenda 2030- Amina

Umoja wa Mataifa umetaja mambo makuu mawili ambayo itazingatia katika kuwezesha nchi wanachama kutekeleza kwa ufanisi Ajenda Mpya ya Miji yenye lengo la kuhakikisha kuwa kila mtu anapata haki sawa na kunufaika na fursa zitokanazo na ukuaji wa miji kiendelevu.

Vita vya Ukraine: Mkuu wa UN awasili kwa mazungumzo Moscow kama mjumbe wa amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza haja ya "kuweka hai maadili ya ushirikiano wa kimataifa" huku vita vya Ukraine vikiendelea na athari zake kote duniani.

Katibu Mkuu wa UN na Rais wa Uturuki wajadili matarajio ya amani ya Ukraine 

 Leo 25 Aprili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mjini Ankara. 

Tukiadhimisha siku ya Malaria, hebu tushikamane kuelekea ulimwengu usio na janga hilo:WHO 

Katika kuadhimisha siku ya malaria duniani, hii leo afisa wa shirika la afya duniani WHO amesema kwamba licha ya janga la COVID-19, mwaka uliopita umeshuhudia "mafanikio muhimu katika kuzuia na kudhibiti malaria." 

Mwai Kibaki alikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Kenya:Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia, serikali na wananchi wa Kenya kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa taifa hilo la Afrika Mashariki Mwai Kibaki. 

Ushirikiano wa kimataifa na diplomasia kwa ajili ya amani unaenda mrama:Guterres 

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya ushirikiano wa kimataifa na diplomasia kwa ajili ya amani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba lengo la siku hii limeanza kwenda mrama.