Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba vita vinapozuka, watu wanakabiliwa na njaa, na kwamba asilimia 60 ya watu wasio na lishe bora duniani wanaishi katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro huku akikumbusha kuwa "Hakuna nchi iliyo na kinga dhidi ya njaa,"